Aya 38 – 49: Juu Ya Vitanda Wameelekeana
Maana
Hakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu.Wala hamtalipwa ila mliyo kuwa mkiyafanya.
Baada ya Mwenyezi Mungu kusema kuwa wakosefu watashirikiana katika adhabu, sasa anawaambia kuwa adhabu yao ni malipo ya yaliyochumwa na mikonoi yao, wala hawatadhulumia hata chembe.
Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliotakaswa. Hao ndio watakaopata riziki maalumu.
Hii ni desturi ya Qur’an, kuwataja wakosefu na adhabu yao kisha kufuatia kuwataja wema na malipo yao. Malipo yenyewe kwa ujumla ni riziki maalum ya Mwenyezi Mungu kwa ajili yao.
Ama ufafanuzi wa riziki hiyo ni kama ifuatavyo:
Matunda, wanayoyatamani, nao watahishimiwa. Kwa sababu matunda na kudharauliwa ni sumu na huzuni. Kuna mithali isemayo: “Niheshimu wala usinilishe”
Katika Bustani za neema, zinazopitiwa na mito. Wako juu ya viti wamekabiliana, wakiangaliana kwa raha na furaha
Wakizungushiwa kikombe cha chemchem. Vijana watawapatia kinywaji cheupe kitamu kwa wanywao, chenye rangi na ladha nzuri. Hakina madhara, Hakiumizi kichwa wala kuleta maumivu wala hakimaliziki.
Neno nazaf likitumika kwenye kinywaji lina maaana ya kumalizika na likitumika kwa mtu lina maana ya kuisha akili yake; ndio maana baadhi ya wafasiri wakasema “Hakiwaleweshi;” yaani kinywaji hakimalizi akili yao.
Na watakuwa nao wanawake wenye macho makunjufu
Matunda, heshima, furaha, watumishi na zaidi ya hayo ni wanawake safi warembo wenye macho makunjufu na mazuri, kama kwamba wao ni mayai yaliyohifadhika. Kuwa kama mayai ni kinaya cha usafi wao na kuwa hawajaguswa na mikono wala kutazamwa na mcho.
Wanawake Na Watumishi
Hivi karibuni nilipata barua kutoka kwa mwananfunzi mmoja wa kike wa Kuwait, ikisema kuwa alikuwa na mazungumzo na rika lake. Yeye akasema kuwa Uislamu haumtofautishi mwanamume na mwanamke.
Wenzake wakampinga na kumwambia kuwa Qur’an imeelezea wazi kuwa Mwenyezi Mungu kesho atawalipa wanaume wema mahurulaini na hakusema vile atakavyowalipa wanawake wema. Kama haki ingelikuwa sawa, basi malipo yangelikuwa ya aina moja. Msichana anasema alishindwa kujibu na akataka nimwandikie ili awakinaishe wenzake.
Majibishano haya mazuri yanatufahamisha kuwa mwanamke ni sawa na mwanamume katika mataminio yake ya kimwili na mapendeleo yake. Na kwamba kupata mume ndio malipo bora zaidi, kama ilivyo kwa mwana- mume kupata mke. Vile vile inatufahamisha kuwa wivu wa mwanamke kwa mwanamume ni kama wa mwanamume.
Basi nikamjibu hivi: “Qur’an imeelezea waziwazi usawa baina ya mwanamume na mwanamke kama msingi wa ujumla. Kwenye hilo inasema:
أَنِّي لَا أُضِيعُ عَمَلَ عَامِلٍ مِنْكُمْ مِنْ ذَكَرٍ أَوْ أُنْثَىٰ ۖ {195}
“Mwenye kufanya mema - mwanamume au mwanamke - hali ya kuwa ni mwenye kuamini, basi hao wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa hata kitobwe cha kokwa ya tende.” Juz. 5 (4:124).
Hakuna mwenye shaka kwamba atakayeingia Peponi atapata kila kinachotamaniwa na nafsi na kuburudisha macho awe mwanamume au mwanamke, kama ilivyoelezwa kwenye (43:71).
Vile vile Qur’an imewataja watumishi kama ilivyowataja Hurulaini. Ilipowasifu Hurulaini kuwa ni kama mayai yaliyohifadhika, pia imewataja watumishi kuwa ni lulu iliyotawanywa, kama iliyosemwa kwenye. (76:19)
Sio mbali kuwa kunyamazia kutaja kuwa mwanamke atalipwa kwa kijana mzuri kumefuata ada na desturi iliyozoeleka kwa watu ya kumzungumzia kijana kuoa na kumuuliza, kwa nini huoi? Lakini hawamuulizi msichana, kwa nini huolewi; kwa vile wanakuwa na haya sana. Wakale walisema: “Ana haya kama msichana.”
Vile vile imesemekana kuwa ladha za Peponi zote ni za kiroho si za kimaada au jinsia, na kwamba kutaja hurilaini, matunda na vikombe ni kama ishara na alama ya ladha ya kimwili kwenye ladha ya kiroho na kwamba viti na vitanda ni kinaya cha cheo na daraja.
فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ {50}
قَالَ قَائِلٌ مِنْهُمْ إِنِّي كَانَ لِي قَرِينٌ {51}
يَقُولُ أَإِنَّكَ لَمِنَ الْمُصَدِّقِينَ {52}
أَإِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَدِينُونَ {53}
قَالَ هَلْ أَنْتُمْ مُطَّلِعُونَ {54}
فَاطَّلَعَ فَرَآهُ فِي سَوَاءِ الْجَحِيمِ {55}
قَالَ تَاللَّهِ إِنْ كِدْتَ لَتُرْدِينِ {56}
وَلَوْلَا نِعْمَةُ رَبِّي لَكُنْتُ مِنَ الْمُحْضَرِينَ {57}
أَفَمَا نَحْنُ بِمَيِّتِينَ {58}
إِلَّا مَوْتَتَنَا الْأُولَىٰ وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ {59}
إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ {60}
لِمِثْلِ هَٰذَا فَلْيَعْمَلِ الْعَامِلُونَ {61}
أَذَٰلِكَ خَيْرٌ نُزُلًا أَمْ شَجَرَةُ الزَّقُّومِ {62}
إِنَّا جَعَلْنَاهَا فِتْنَةً لِلظَّالِمِينَ {63}
إِنَّهَا شَجَرَةٌ تَخْرُجُ فِي أَصْلِ الْجَحِيمِ {64}
طَلْعُهَا كَأَنَّهُ رُءُوسُ الشَّيَاطِينِ {65}
فَإِنَّهُمْ لَآكِلُونَ مِنْهَا فَمَالِئُونَ مِنْهَا الْبُطُونَ {66}
ثُمَّ إِنَّ لَهُمْ عَلَيْهَا لَشَوْبًا مِنْ حَمِيمٍ {67}
ثُمَّ إِنَّ مَرْجِعَهُمْ لَإِلَى الْجَحِيمِ {68}