Aya 26 – 29: Tumekufanya Uwe Khalifa Ardhini
Maana
Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya uwe Khalifa ardhini.
Kila mtu aliyeko, au atakayekuweko, ardhini basi huyo ni khalifa wa Mwenyezi Mungu ardhini; kwa maana yakuwa ana majukumu mbele ya Mwenyezi Mungu ya kufanya mambo ya heri duniani na Akhera katika maisha haya.
Hayo ndio maana ya ukhalifa ardhini kwa hali yoyote ile; isipokuwa watu wanatofautiana kulingana na majukumu yenyewe; ambapo kila mmoja anatakiwa atekeleze kulingana na uwezo na wadhifa wake.
Kwa kuwa wadhifa wa manabii ni kutoa bishara na hadhari, ili watu wasiwe na hoja mbele ya Mwenyezi Mungu, basi imekuwa ni wajibu kwao kuwahukumu watu kwa haki na wengine wawasikilize wao.
Basi wahukumu watu kwa haki, wala usifuate matamanio, kwa sababu unabii uko hivyo kimaumbile.
Kwa maneno mengine ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anamchagulia wahyi wake yule anayeiamini haki na kuitumia na inakuwa ni muhali kwake kukosea.
Yakakupoteza Njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika wanaopotea Njia ya Mwenyezi Mungu, watapata adhabu kali kwa sababu ya kusahau kwao Siku ya Hisabu.
Muovu zaidi katika watu ni yule mwenye kumhalifu Mola wake na akafuata matamanio yake. Kuna Hadith isemayo: “Hakika ninalolihofia zaidi kwenu ni hawaa na tamaa nyingi. Hawaa inaipinga haki na tamaa nyingi inasahauliza akhera.”
Na hatukuziumba mbingu na ardhi na viliomo kati yake bure.
Lau katika kuumbwa mbingu na ardhi kungelikua na chembe ya mchezo au hivi hivi tu, basi ulimwengu usingeendelea na nidhamu kwa mamilioni ya miaka.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 4 (3:191).
Hiyo ni dhana ya waliokufuru. Ole wao waliokufuru kwa Moto.
Hiyo inaashiria kuwa hakuna tofauti kati ya aneyepinga kuweko Mwenyezi Mungu kabisa na yule anayekubali, lakini akapinga kuweko hekima katika kuumba kwake. Kwa sababu dalili zake ni wazi na alama zake ziko kweupe.
Imam Ali (a.s.) anasema: “Amekadiria aliyoumba akapangilia makadirio yake; akapangilia akafanya kwa uangalifu mipangilio yake; akaelekeza kwa maelekezo yake, lakini hakupetuka mpaka wa cheo chake wala hakupunguza ukomo wa lengo lake.”
Je! Tuwafanye walioamini na wakatenda mema kama wafisadi katika ardhi? Au tuwafanye wenye takua kama waovu?
Tofauti baina ya mwema na mfisadi na baina ya mwenye takua na muovu ni sawa na tofauti baina ya kipofu na mwenye kuona. Umetangulia mfano wake katika Juz. 7 (5:100) na Juz. 7 (6:50).
Katika kitabu Ahkamul-qur’an cha Kadhi Abi Bakri, ambaye ni maarufu kwa jina la Ibnul-arabiy, amesema: “Aya hii iliwashukia bani Hashim; na kwamba walioamini na kuwa na takua ni Ali bin Abi Twalib, ndugu yake Ja’far, Ubayda bin Tufayl, Al-harth bin Tufayl, Ummu ayman na wengineo, na kwamba wafisadi na waovu ni Bani Abd Shams.
Hiki ni Kitabu, tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili.
Hapa anaambiwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.). Kitabu ni Qur’an, nayo ina baraka kwa kila mwenye kuiamini, ni dawa ya ukafiri na hulka mbaya na ni uokovu wa shirki na maangamizi. Kwenye Nahjul-Balagha imeelezwa: “Itakeni nasaha kwa nafsi zenu na mzituhumu rai zenu kwayo na mtake uokofu wa hawa zenu ndani yake.”
وَوَهَبْنَا لِدَاوُودَ سُلَيْمَانَ ۚ نِعْمَ الْعَبْدُ ۖ إِنَّهُ أَوَّابٌ {30}
إِذْ عُرِضَ عَلَيْهِ بِالْعَشِيِّ الصَّافِنَاتُ الْجِيَادُ {31}
فَقَالَ إِنِّي أَحْبَبْتُ حُبَّ الْخَيْرِ عَنْ ذِكْرِ رَبِّي حَتَّىٰ تَوَارَتْ بِالْحِجَابِ {32}
رُدُّوهَا عَلَيَّ ۖ فَطَفِقَ مَسْحًا بِالسُّوقِ وَالْأَعْنَاقِ {33}
وَلَقَدْ فَتَنَّا سُلَيْمَانَ وَأَلْقَيْنَا عَلَىٰ كُرْسِيِّهِ جَسَدًا ثُمَّ أَنَابَ {34}
قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي وَهَبْ لِي مُلْكًا لَا يَنْبَغِي لِأَحَدٍ مِنْ بَعْدِي ۖ إِنَّكَ أَنْتَ الْوَهَّابُ {35}
فَسَخَّرْنَا لَهُ الرِّيحَ تَجْرِي بِأَمْرِهِ رُخَاءً حَيْثُ أَصَابَ {36}
وَالشَّيَاطِينَ كُلَّ بَنَّاءٍ وَغَوَّاصٍ {37}
وَآخَرِينَ مُقَرَّنِينَ فِي الْأَصْفَادِ {38}
هَٰذَا عَطَاؤُنَا فَامْنُنْ أَوْ أَمْسِكْ بِغَيْرِ حِسَابٍ {39}
وَإِنَّ لَهُ عِنْدَنَا لَزُلْفَىٰ وَحُسْنَ مَآبٍ {40}