read

Sababu za Uchelewesho Katika Uandishi wa Hadith

Inafahamika vyema kabisa kuwa Mtume s.a.w.w., kuanzia mwanzoni kabisa mwa Utume wake, aliupatia umuhimu zaidi (na kusisitiza) kuhusu uandishi wa Qur’an (kama hatua ya kinga dhidi ya kughushi na uongo). Kimatokeo Qur’an ikawa ipo mbali na makosa au mabadiliko (tahrif).
Hata hivyo, katika upande wa Hadith (kwa mujibu wa imani yetu ni kweli kwamba) baadhi ya Ahadith yaliandikwa katika zama za uhai wa Mtume s.a.w.w., lakini baada ya kuondoka kwake (kufariki) kutoka dunia hii, sio kwamba tu kuwa haukupewa umuhimu hiyo kazi ya uandikaji wa Hadith, bali iliweza hata kupingwa na Upingamizi huo ulisababisha matatizo mengi kuhusiana na Hadith, ambayo tutayaona hapo mbeleni.

Uchelewesho huo wa kuziandika Hadith na matokeo yenye hatari yalifanya kikundi kimoja kumtupia lawama na'udhubillah Mtume s.a.w.w. Wao walitambua wazi kuwa upingamizi wa uandishi wa Hadith iwapo itatokea kwa Mtume s.a.w.w., basi haitaweza kulaumiwa, kwani Mtume s.a.w.w. hawezi kulaumiwa; hata hivyo, iwapo wataielezea kwa wengine basi itatoboa udhaifu wao. Kwa hivyo, walimwelekezea Mtume s.a.w.w. kuwa ndiye aliyekataza kuandikwa kwa Hadith.