Mtunzi Na Habari Zake
Kitabu hiki cha Sadaka ambacho kipo mikononi mwenu, Hadith zake zimetolewa kutoka Wasa’il as-Shi’ah na tunaona vyema kuwaleteeni habari chache kuhusu kitabu na mtunzi wake.
Sheikh Hurri ‘Aamili baada ya jitihada zake nyingine kwa muda wa miaka ishirini mfululizo amekigawa kitabu hicho katika sehemu sita katika fani mbalimbali na kuzigawia Hadith kimpangilio mzuri kabisa na kwa hakika anastahili pongezi kubwa sana kwa jitihada zake zote katika kuzipanga Hadith kimpangilio mnavyouona katika kitabu hiki pia.
Mwandishi wa Al-Mizaan fi Tafsir al-Qur'an yaani As-Sayyid Muhammad Hussein Tabatabai kuhusu Wasa’il as-Shi’ah anaandika:
Kwa hakika kitendo hicho ni kipeo cha hali ya juu kabisa katika maswala ya Fiqh na Mafuqahaa na Mujtahidiin wanakitegemea sana. Wao katika kutoa mafatwah zao wanakitumia na kukitegemea sana kitabu hiki ambacho kinawafaidisha na hawana shaka yoyote kwenye kitabu hiki. Mambo yote ambayo yamezungumzwa humu kwa hakika yana mapana yake, kwa hakika kulingana na zama zao hizo, mpangilio na utaratibu uliotumika kunasaidia na wenye manufaa sana. Kwa hakika inatubidi sisi tujali na kutekeleza na kuipa muhimu sana matamshi na maneno matakatifu yaliyozungumzwa na watu watukufu kabisa.
Sheikh Hurri ‘Aamili alikuwa ni mwandishi yaani ni mtu mwenye habari, na ni mmoja wa waandishi wa vitabu vinne vya kutegemewa kabisa ambavyo vimekwisha kuelezwa hapo nyuma. Kwa hakika katika zama zetu hizi kuna pengo kubwa sana la ma’ulamaa kama hao ambalo haliwezi kuzibwa; kwa hakika athari ya mapengo hayo yanaonekana katika zama zetu na zile zitakazo kuja kwa sababu mapengo yamebakia wazi, yanaongezeka na ma’ulamaa wengi wametumia kazi ya Bwana Hurri ‘Aamili kama vile Sayyid Abul Qasim Al-Khui ametumia katika Mu’jamur Rijaal na kumtaja kuwa Bwana Sheikh ‘Aamili alikuwa ni mtu wa maswala ya habari pia. Hivyo hivyo hali kadhalika Sheikh ‘Aamili alizaliwa katika Jabal ‘Aamil kijiji kimoja kijulikanacho kama Mashgharah (Mwezi wa Rajab mwaka 1033 Hijriyyah) na amefariki na amezikwa Mash-had al-Muqaddas katika mwaka 1104 Hijriyyah.
Katika sehemu mwisho ya Wasa’il as-Shi’ah ‘Aamili ana andika kuhusu Allama Majlisi a.r. ana andika kuwa: Yeye ni mwisho katika wale waliokuwa wamenipa idhini, nami nilimpa idhini.
Mbali na kitabu cha Wasa’il as-Shi’ah, Sheikh ‘Aamili ameandika vitabu vingine ishirini na sita ambavyo vingi vyake vina Juzuu mbalimbali. Kwa hakika mwanga wake huo mkubwa alioutoa kwa ajili ya madhehebu ya Ahlul Bayt a.s. ni mkubwa sana na wenye kustahili kusifiwa na kupewa heshima zote.
Tunaomba Allah swt awajaalie kila la heri Ma’ulamaa wakubwa waliojitolea mhanga kuinusuru dini hii tukufu ya Islam.
Kwa hakika kitabu hiki cha Sadaka ni sehemu moja tu ndogo au tunaweza kusema ni sura mojawapo katika Juzuu ishirini za Wasa’il as-Shi’ah katika sura inayoitwa Kitabu cha Zakah. Mkiangalia kazi yake yote hiyo kwa hakika hamtakuwa na la kusema. Na sura hii inaitwa Kitabu cha Sadaka ambacho kinazungumzia mambo juu ya Sadaka na humo zipo sura hamsini na nne; sasa fikiria kama yeye kwa swala (mada) moja dogo hili amechukua kwa hakika uzito mkubwa kama huo Je! tufikirie kazi yote hiyo itakuwa imechukua uzito (umuhimu) gani?
Kwa hiyo ndugu msomaji sababu ya kupenda kuchukua maudhui haya ni mambo mawili,
• Kwanza kabisa ni kuweza kuwadhihirishia na kuwaonyesha mchango wa Ma’ulamaa wa Kishi’ah katika ilimu hii ya Hadith na
• vile vile kuteketeza uvumi kuwa Mashi’ah wanaikubali Qur'an Tukufu lakini hawakubali na hawana Hadith zozote wao na kwa hakika hilo ndilo litakalo kuwa jibu letu.
Kwa hakika ukiweza kuangalia utaona kuwa ilimu ya Hadith imehifadhiwa na kuendelezwa na hii Madrasah ya Ahlul Bayt a.s. ambapo kwa wengine jambo hili halikupewa uzito wala tahadhari ya aina yoyote ile. Leo ukiangalia katika ulimwengu wa Masunni utaona kuwa vitabu vyao vilivyopo wamshukuru ‘Umar ibn ‘Abdul Aziz na kama akiwa kiongozi mtawala asingetia msisitizo katika swala hili basi hawa watu ambao wamejitenga na Ahlul Bayt a.s. wangekuwa hawana chochote, hazina yao ingekuwa tupu kabisa.
Vile vile mtarjumu wa kitabu hiki ambaye yeye ametokea Umma huu na amesomea, hivyo ameona afadhali kuwa kazi aifanye ili aweze kuleta mbele ya umma huu na kwa ajili ya manufaa ya wana-‘umma huo kwa hivyo itasaidia pia kumtaarufisha mwandishi wa kitabu hiki.
Sote kwa pamoja tunaomba kwa Allah swt nguvu zetu na jitihada zetu hizi azikubalie. Iwapo kumetokezea au kumebakia kasoro zozote katika kutarjumu basi tunamwomba Allah swt atusamehe na ninawaomba Wanazuoni na wenye ilimu wajaribu kusaidia kurekebisha kwa sababu katika kukitarjumu kitabu hiki hapakuwapo na matayarisho kamili kuanzia awali.
Na kazi hii imefanywa kwa nia njema kwa matarajio kuwa itatumika kwa nia njema na itafaa kutupeleka mahala pema, Inshallah.
Naomba kazi yangu hii niiweke mbele kwa idhini ya Allah swt, na kuiweka mbele ya Al Imam Muhammad Sahibuz-Zamaan a.s. iwe ni kama zawadi kwake.