read

Utambulisho wa Ma’sumiin a.s.

Katika Ahadith: Kuniyyat na Alqaab

Mara nyingi tunaposoma vitabu vya riwaya tunapata majina mengine yaliyotofauti na majina ya asili. Hivyo tunaona katika Ahadith kuwa Ma’asumiin a.s. wanatambulishwa kwa majina yanayoitwa Kuniyyat au Ilaqab, kwa mfano: Qala Abul Hasan ( yaani amesema Abul Hasan ) au Qala Abu ‘Abdillah (yaani amesema Abu ‘Abdillah) n.k. na hapo ndipo tunakuwa hatuelewi ni Ma’sum a.s. yupi ambaye amesema hayo.

Waarabu wanayo desturi ya kuwaita wazee wao si kwa majina yao bali kwa majina mengineyo yaani Kuniyyat au Alqaab. Hivyo inatubidi tupate ufafanuzi zaidi kuhusu majina hayo yanayotumiwa kwa ajili ya Ma’sumiin a.s zaidi ya mara moja. Na hivyo Ma’ulamaa wetu wametuelewesha ilivyo sahihi kabisa.

Wakati wa kujaribu kufafanua juu ya Laqab au Kuniyyat kunatiliwa maanani kuhusu maneno na maana ya Hadith, zama za kusemwa na habari za wale wanaoziripoti, ndipo hapo panapoweza kutambuliwa kwa Alqaab au Kuniyyat katika Hadith hiyo kunatambulishwa Ma’sumiin a.s. yupi.

Hivyo kuelezea hayo na mengineyo, maelezo yafuatayo yatasaidia kutoa mwanga katika swala hili kwa ujumla:

1. Abul Qasim - Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Mtume Muhammad s.a.w.w. na Imam al-Mahdi a.s. Iwapo kutaripotiwa riwaya kuwa Abul Qasim tu, basi ijulikane kuwa ni Imam al-Mahdi a.f.

2. Abu Muhammad - Zipo Hadith chache mno zinazojulikana kuwa Imam Hasan a.s. Hata hivyo hiyo ndiyo Kuniyyat yake.

3. Abu ‘Abdillah - Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Imam Hussein a.s na vile vile inatumika kwa ajili ya Imam Ja’afer as-Sadiq a.s.

4. Abul Hasan - Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. , Imam Musa ibn Ja’afer a.s., Imam Ali ibn Musa al-Ridha a.s. na Imam Ali an-Naqi a.s. Iwapo kutakuwapo na Abul Hasan tu katika riwaya, basi kutatambuliwa Imam Musa ibn Ja’afer a.s. Na iwapo kutaandikwa Abul Hasan Thani (Abul Hasn wa pili) basi kutakuwa kumefanywa ishara ka Imam ‘Ali ar-Ridha a.s. na pale panapoandikwa Abul Hasan Thalith (Abul Hasan wa tatu) basi tujue kuwa kunamaanishwa Imam ‘Ali an-Naqi a.s.

5. Abu Muhammad - Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Imam Hasan a.s., Imam Zaynul Aabediin a.s na Imam Hasan al-‘Askari a.s. lakini iwapo kutaandikwa riwaya kwa Abu Muhammad tu tutatambua kuwa riwaya hiyo ni kutoka Imam Hasan al-‘Askari kwa sababu riwaya za Imam Zaynul Aabediin a.s. zinatajwa kwa jina lake tu, bali zipo riwaya chache mno tu kwa Kuniyyat yake.

6. Abu Ibrahim - Katika Hadith, Kuniyyat hii inatumika hasa kwa ajili ya Imam Musa ibn Ja’afer a.s.

7. Abu Is-Haq - Kuniyyat hii inatumika kwa kumtambulisha Imam Ja’afer as-Sadiq a.s.

8. Abu Ja’afer - Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Imam Muhammad al-Baqir a.s. na Imam Muhammad Taqi a.s

Lakini iwapo kutakuwapo na Abu Ja’afer tu au Abu Ja’afer Awwal, (Abu Ja'afer wa kwanza) basi ijulikane kunamaanishwa kwa Imam Muhammad al-Baqir a.s.

Na iwapo kutaandikwa Abu Ja'afer Thani (Abu Ja'afer wa pili) basi kutambuliwe kuwa ni Imam Jawad a.s.

Kwa mara chache mno Abul Hasan inatumika kwa ajili ya Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. lakini mahala pengi mno kunatumika Kuniyyat yake mahsusi ya Abul Hasanain.

Alqaab

Wakati pale utakapoona riwaya zinanakiliwa kutoka kwa ‘Aalim, Sheikh Faqih au ‘Abdi Salih, basi mutambue kuwa kunamaanishwa kwa
Al Imam Musa al-Kadhim a.s.

Vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anajulikana kwa alqaab zifuatazo: Sheikh, Abu ‘Abdillah, Faqih na ‘Aalim.

‘Allamah Majlisi a.r. anasema kuwa mahala pengi mno katika riwaya kunapotajwa Faqih basi kunamaanishwa kwa Imam ‘Ali an-Naqi a.s. na kwa mara chache mno kunatumika Jawallaij kwa ajili ya Imam Hasan al-‘Askari a.s na Al Imam Muhammad Sahibuz-Zamaan a.s.

Naqi, Mazii, Sahibul ‘Askar na Hajul kunamaanisha Imam Hasan al-‘Askari a.s.

Sahib na Sahibuddaar zinatumika makhsusi kwa ajili ya Imam al-Mahdi a.s. Lakini Sahibun Nahiyah inapokuja, basi kwa mara nyingine hutumika kwa ajili ya Imam ‘Ali an-Naqi a.s. au Imam Hasan al-‘Askari a.s. ‘Allamah Majlisi anasema kuwa mara nyingine katika Ahadith hutumika maneno Ghaib, ‘Alil au Gharim basi inatubidi kuelewa Imam al-Mahdi a.s.

Iwapo kutakuwapo bi ahadihima (kwa mojawapo) basi itatubidi tuelewe kuwa ni ishara kwa Imam Muammad al-Baqir a.s. au Imam Ja'afer as-Sadiq a.s.

Na iwapo tutakuwa bi ‘Askariyyen, tuelewe kuwa ni Imam Ali an-Naqi a.s. na Imam Hasan al -‘Askari a.s.

Vile vile iwapo tutaona bi Kadhmain basi kunamaanishwa Imam Musa al-Kadhim a.s. na Imam Mahammad at-Taqi a.s.

Kwa mukhtasari, zipo alqaab nyingi ambazo zinajulikana kimakhsusi kwa ajili ya Ma’sumiin a.s. kama vile Amir al-Mu’miniin, Mujtaba Shahid, Zaynul Aabediin, Baqir, Sadiq, Kadhim, Ridha, Jawad, Hadi, ‘Askari, na Sahib uz Zamaan (salaam ziwe juu yao wote).