Aina Za Ahadith
Sayyid Ibn Taus a.r. (amefariki 673 Hijriyyah) na ‘Allamah Hilli a.r. (amefariki 726 Hijriyyah) kwa juhudi zao, wao wamefanikiwa kutuletea kanuni nne kuu zijulikanazo usul-i-‘arbi’ah ambazo ni kama zifuatazo:
1. Hadith Sahih
Rawi wote lazima wawe waaminifu na Shia Ithna-Asheri na riwaya hizo ziwe zikifika hadi kwa Ma’sumiin a.s.
2. Hadith Hasan
Riwaya ambazo Rawi wake ni Mashi’ah na ambapo hapakufanywa uchunguzi wowote juu ya uadilifu wao.
Hadith kama hizo zinajulikana kama hasan kwa sababu Rawi amepokelewa kwa misingi ya husnu-dhan yaani kwa dhana njema.
3. Mutawath-thaq
Yaani Rawi wote wawe wakiaminiwa lakini miongoni mwao si wote ambao ni Mashi’ah.
4. Dhaif
Ni riwaya zile ambazo hazina sifa hata mojawapo za hapo juu.
Tanbih lipo jambo moja la kuzingatia, kuwa Ma’ulamaa wanakubaliana na Hadith zilizo Sahih, Hasan na Muwath-thiq. Ama kuhusu Hadith zilizo dhaif ni kwamba iwapo atayamkinika kuwa Rawi hao si watu wa kutegemewa lakini maelezo na maana yake ni sawa na maana ile ya Ma’sumiin a.s. na katika sura hii, itaweza kukubalika, na wakati Ma’ulamaa wanaozisimulia basi nia yao huwa juu ya Hadith, bali huwa ni kutoa ushahidi tu.