read

Madondoo juu ya Sadaka

Hapa nitapenda kuzungumzia machache kuhusu Sadaka
Sadaka inalipia madeni na kuongezea neema kwetu,

Sadaka inatuepusha na mauti katika hali mbaya

• Siku ya Qiyama kutakuwa na jua na joto kali mno, lakini Mu’min atakuwa katika kivuli, nacho ni Sadaka aliyokuwa akiitoa.

• Toeni Sadaka asubuhi na mapema, ili balaa na matatizo yasiwafikieni katika siku nzima.

• Muwatibu wagonjwa wenu kwa kutoa Sadaka

• Kutoa Sadaka ni afadhali kuliko kumnunua mtumwa na kumfanya huru

• Mtu mmoja alifiwa na watoto wawili, alibakiwa na mmoja. Akashauriwa kutoa Sadaka. Toeni Sadaka kwa mikono yenu wenyewe kwani hamtakufa kifo kibaya na balaa zaidi ya 70 zitaepukwa na pia tutajiepusha na mitego 70 ya Shaitani, kwani Shaitani yupo anasema, “Usitoe Sadaka.” Je! tutamwitikia Shaitani ?

• Toeni Sadaka hata kama ni tonge moja ya tende na kama hiyo pia hamuwezi basi toeni punje moja ya tende.

Sadaka inatuepusha na balaa 70 ambamo kuna magonjwa, madhara ya moto, kuzama maji, kuangukiwa na kufunikwa na majumba yanayo poromoka na kubomoka na kutokuwa masikini.

• Unapokuwa na hofu ya kuibiwa, kuungua moto n.k. basi toa Sadaka.