read

2. Msaada kwa Waislamu ni Afadhali kuliko Hijja ya Sunnah

Kusaidia familia ya waislamu wenye shida ni afadhali kuliko kwenda hijja zilizo sunnah na kuwafanya huru watumwa.

1. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema kuwa:
“Iwapo mimi nitakwenda Hijja moja basi afadhali niwafanye huru watumwa kumi, lakini iwapo mimi nitajichukulia jukumu la kuwalisha familia ya Waislamu ambao wanashida ya chakula na ambao wanaishi kwa njaa nikawamalizia shida zao, nikawavalisha nguo wale ambao hawana nguo, na nikawarudishia heshima yao miongoni mwa watu, basi mimi ninaona jambo hili ni afadhali na bora zaidi kuliko hata kwenda kuhiji Hijja sabini.”

2. Al Imam Musa al-Kadhim a.s. aliijiwa na mtu mmoja na aliyeuliza,
“Ewe mwana wa Mtume wa Allah! Mimi ninazo pesa na utajiri Je! ni jambo gani afadhali nitoe sadaka au nimnunue mtumwa na kumfanya huru?”

Kwa hayo Al Imam Musa al-Kadhim a.s. alimjibu kuwa:
“Mimi ninaonelea kuwa kutoa Sadaka ni afadhali zaidi.”

3. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:
“Siku moja Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwuliza Maimuna binti Harun, Je! Kijakazi wako amekuwaje? Akasema Maimuna kwa hayo alimjibu Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., ‘Ewe Mtume wa Allah! Mimi nimemfanya huru.’

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwambia “Iwapo kama wewe ungelichukua jukumu la kumlisha, kumtunza, kumsaidia na kumwonea huruma basi ingekuwa afadhali zaidi.”