read

3. Kuwatolea Wagonjwa Sadaka ni Sunnah

1. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:
“Muwatibu wagonjwa wenu kwa Sadaka, na muzuie maafa kwa kuomba dua na kutoa sadaka muongezee riziki zenu zipanuke, na kwamba Sadaka inawaepusheni na mitego ya mashetani sabini.”

2. Siku moja walikuja wagonjwa wakilalamikia magonjwa yao mbele ya Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., naye akawaambia:
“Nendeni mtoe Sadaka kwa ajili ya magonjwa yenu na mtapona, iwapo mtu atatoa Sadaka kwa kile akitumiacho kwa siku ya dharura yake, basi Allah swt huahirisha hata kifo chake na vile vile humwepusha na ajali mbaya.”