read

6. Kutoa Sadaka Kila Mara na kwa Wingi ni Sunnah

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:
“Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa alimusia Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.; Ewe Ali! Ninakufanyia usia wa mambo mema machache na uyakumbuke vyema".

“Ewe Allah swt umsaidie 'Ali” Baada ya hapo wakati akifanya usia, Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alisema: “Ama kuhusiana na sadaka, tafadhali usiwe na mnun’guniko wowote. Utoe kiasi kwamba mpaka uhisi kwamba wewe umefuja mali yako, lakini utambue wazi kuwa hiyo sio ufujaji bali hiyo umetoa katika njia ya Allah swt.”