11. Waombaji Wanatakiwa Waridhike kwa Kile Wanachopata
Waombaji wanatakiwa waridhike kwa kile wanachopata, ni sunnah kuwaongezea wale walioridhika na kutowajali wale wasioridhika.
Siku moja Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alikuwa Mina pamoja na Ma-Sahaba wake, wakila zabibu. Mara akatokezea mtu mmoja na akaomba. Basi Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kwa mkono wake akachukua fungu moja la zabibu akampa basi huyo akakataa kupokea, akisema “mimi sitaki zabibu hizi bali ninataka pesa tasilimu kama zipo ndio nichukue”.
Basi kwa kusikia hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamwambia “Allah swt atakuzidishia” na Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. hakumpa chochote, baada ya muda si muda huyo mwombaji tena akarudi kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. na akamwambia Imam a.s. “Nipe zile zabibu ulizokuwa ukitaka kunipa.” Na Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamwambia Allah swt atakutafutia njia yake, pamoja na hayo Imam a.s. hakumpa chochote.
Wakati bado wakiwa wamekaa akatokezea mtu mwingine kuja kuomba, na Imam a.s. alitoa mbegu tatu tu za zabibu akampa huyo mwombaji. Mwombaji huyo alianza kumshukuru Allah swt kwa kumjaalia riziki hiyo na akaonyesha shukrani kwa ujumla. Kwa kusikia hayo Imam a.s. alichota mikono ya zabibu miwili akampa na hapo tena huyo mwombaji akaendelea kumshukuru Allah swt zaidi na zaidi. Kwa kusikia hayo tena Imam a.s. akamwambia mtumwa wake kama tuna pesa zozote zile tulizo nazo kwetu mpe huyo. Na huyo mfanyakazi wa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kwa amri yake alimpa Dirham Ishirini alizokuwa nazo. Mwombaji akiwa anachukua Dirham akasema: ‘Ewe Allah swt! Nakushukuru mno sana na hakuna mwingine wa kushirkishwa nawe.
Kwa kusikia hayo Imam a.s. nguo aliyokuwa amejifunika akampa huyo mwombaji na huyo mwombaji baada ya kuivaa na kujifunika na hiyo nguo akamshukuru Allah swt ambaye amemjaalia nguo ya kujifunika. ‘Ewe Aba ‘Abdillah! Allah swt akulipe kila la heri.
Na baada ya kusema hayo akaondoka zake. Kwa kuona haya Ma-Sahaba wakamwambia Imam a.s. kuwa kila alivyoendelea yeye kumsifu Allah swt ndivyo wewe ulivyoendelea kumpa na kama asinge omba kwa kutaja jina la Al Imam a.s. lazima ange endelea kumpa chochote zaidi ya hayo.”