read

12. Ufahamu ya Muda au Masaa ya Kutoa Sadaka

Asubuhi na mapema na usiku unapoingia na saa zinazokuwa mbaya unapotoka nje basi mtoe sadaka.

1. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:
“ Mimi nilinunua ardhi pamoja na mtu mmoja. Mtu huyo huyo alikuwa ni mnujumi, kwa hiyo yeye kila alipokuwa akipiga mahesabu yake na elimu ya nyota yake aliyokuwa nayo, alikuwa akiangalia saa nzuri ndipo alipokuwa akienda shambani mwake, nami bila kujali kama saa mbaya nilikuwa nikienda shambani mwangu, na sisi tulipokuwa tayari basi ardhi au sehemu yangu ikawa na faida zaidi kuliko sehemu yake.

Kwa hivyo yeye bila kusita katika hali ya kustaajabisha aliniambia mimi sijawahi kuona kama hivi. Mimi kila saa zilizokuwa nzuri nilikuwa nikija shambani mwangu. Na wewe bila kujali saa nzuri au mbaya ulikuwa ukija kwenye shamba lako. Sasa itakuwaJe! mimi nipate hasara au kasoro?

Basi Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamjibu ngoja nikuambie hadithi moja ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliyesema kuwa:
‘Mtu yeyote anayetaka Allah swt amwepushe na maovu na mabaya ya siku nzima basi yeye aianze siku yake kwa kutoa Sadaka, na yeyote anayetaka ajiepushe na balaa na maovu ya usiku basi yeye usiku unapoingia atoe Sadaka na ujue kwamba mimi daima ninapotoka nyumbani mwangu huwa ninatoa Sadaka. Kwa hivyo kufanya biashara na Allah swt hivi afadhali zaidi kuliko elimu yako ya nyota na kupiga ramli.”

2. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema :
“ Mtoe Sadaka usiku kwa sababu huiondoa ghadhabu ya Allah swt, husamehe madhambi mazito, na hukusababishia hesabu zako siku ya Qiyamah zikaenda vizuri. Kutoa Sadaka katika siku kunaongezea mali yako na kuilinda na unaufanya umri wako uwe mrefu.”

3. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:
“ Kwa kutoa Sadaka yaani kunapokucha, kunayeyusha madhambi kama vile chumvi inavyoyeyuka katika maji. Na kunapotolewa Sadaka usiku basi kunaondoa ghadhabu za Allah swt.”

4. Ibn ‘Abbas amesema kuwa: Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu, Sura Al-Baqarah, 2 Ayah 274:
‘Wale wanao toa mali zao usiku na mchana, kwa siri na dhaahiri, wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi; wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika.’

“Aya hiyo imeteremshwa makhsusi kwa ajili ya Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kwa sababu yeye alikuwa anazo Dinar chache ambazo wakati wa usiku akizitoa kama sadaka, yaani baadhi ya Dinar hizo wakati wa usiku na baadhi wakati wa mchana na zinginezo katika hali ya siri na zinginezo zikiwa ni dhahiri alizokuwa akitoa Sadaka katika njia ya Allah swt.”