13. Ni Vyema Kutoa Sadaka Kifichoficho Kuliko Kidhahiri
1. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa akisema kuwa:
“Kwa kutoa Sadaka kifichoficho ghadhabu za Allah swt hupoa.”
2. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:
“Sadaka inayotolewa kidhahiri, basi kuliko hiyo Sadaka inayotolewa kifichoficho ni afadhali zaidi.”
3. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. siku moja alisema kuwa:
“Mambo yanayomfikisha mtu moja kwa moja kwa Allah swt kama kipitio (au Wasila) ni imani. Na baada yake ni kuwatendea mema ndugu na majamaa zake; mtu ambaye inaongezea baraka katika mali yake na umri wake ukawa mrefu na Sadaka inayotolewa kifichoficho inamfanya huyo mtu asamehewe madhambi yake, na madhambi aliyokuwa yamemgadhabisha Allah swt kwa sababu ya kutomtii, yanabadilishwa kuwa mema na baadaye ni tabia njema na uwema, mambo ambayo yanaepusha ajali mbaya na inamfanya huru mtu katika makucha ya udhalilisho.”
4. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:
“Kwa kutoa Sadaka kidhahiri kunaondoa aina sabini za balaa lakini kwa kutoa Sadaka kifichoficho kunamfanya mtu anusurike na ghadhabu za Allah swt.”
5. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema kuwa:
“Baba yake Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. kila siku usiku alikuwa akitoka nyumbani pamoja na kifurushi cha fedha mgongoni mwake na mara nyingine alikuwa akichukua kifurushi cha vyakula na alikuwa akiwaendea wale wenye shida na dhiki.
Wakati akiwapelekea misaada hii majumbani mwao Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. alikuwa akiufunika uso wake ili wasiweze kumtambua ni nani huyu anayewafikishia misaada mpaka majumbani mwao.
Wakati Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. alipofariki ndipo hapo ikajulikana hawa wanaosaidiwa wenye shida hawapati misaada waliyokuwa wakipata, ndipo hapo wakajua kuwa aliyekuwa anawasaidia mpaka milangoni mwao alikuwa si mtu mwingine bali ni Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s . vile vile wakati Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. alipolazwa wakati wa kuoshwa baada ya kufariki kulionekana mabegani mwake na mgongoni mwake alama zilikuwa zikionyesha kuwa alikuwa akibeba mizigo mizito kwa muda mrefu.
Na katika kipindi kimoja cha baridi kali sana yeye alikuwa amejifunika nguo ambayo ilikuwa inamsaidia asiisikie makali ya baridi wakati alikuwa ametoka nje ya nyumba anakwenda mahala fulani. Njiani alikutana na mtu ambaye alimwomba nguo hiyo ili naye aweze kujistiri na kujizuia dhidi ya makali ya baridi iliyokuwapo. Kwa maombi hayo Al Imam Zaynul 'Aabediin a.s. alimpa hiyo nguo naye akabaki bila nguo ya kujifunika au kujizuia na baridi. Vile vile Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. alikuwa kila mwaka akijifunika nguo ya kujizuia baridi na kipindi kilipokwisha alikuwa akiiuza na fedha zake zote zilizokuwa zikipatikana alikuwa akitumia katika kuwasaidia wenye kuhitaji misaada.”
Vile vile Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. alisema kuwa:
“Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. alikuwa akiwasaidia na kuwalisha na kuwatunza familia zaidi ya mia moja katika mji wa Madina. Na alipokuwa akikaa kula, mayatima, wazee, wagonjwa na masikini walikuwa wakikaa kula naye pamoja na Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s., na vile vile alikuwa akiwafungia vyakula kwa ajili ya kuwachukulia wale waliokuwa majumbani mwao au kama baba ni mzee alikuja kula huko basi alifungiwa chakula awapelekee mke na watoto wake nyumbani.
Vile vile yeye yasemekana kuwa alikuwa hakai kula pamoja na mama yake juu ya meza moja ya chakula na watu walipomwambia ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. wewe ni kigezo cha tabia njema na mfano bora katika Waislamu! Je! kwanini hukai pamoja na mama yako wakati wa kula chakula?.
Al Imam Zaynul 'Aabediin a.s. aliwajibu kuwa,
“Mimi sikai na mama yangu kwa sababu yawezekana mama yangu akiangalia chakula moja labda akataka kuchukua na wakati huo mkono wangu ukawa mrefu kwenda kuchukua chakula hiki, itakuwa kweli hiyo ni kitovu cha nidhamu na ndio maana yake ninajiepusha kukosa nidhamu mbele ya mama yangu.”
6. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema kuwa:
“Mtu anapotoa Sadaka ya chakula kwa ajili ya kuwapa masikini na mafakiri basi mujue kuwa aina hiyo ya Sadaka huondoa ufakiri na humwepusha mtu na kumuondolea ufakiri, na kuurefusha umri wake na humwepusha na aina sabini za vifo vya kutisha (ajali mbalimbali).”
7. Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:
“Siku ya Qiyamah wakati kutakuwa na jua kali lichomalo basi watu aina saba watakuwa wamepewa kivuli na Allah swt na mmoja wao ni yule anayetoa Sadaka ya vyakula kiasi kwamba mkono wa kushoto haupati habari kuwa mkono wa kulia umetoa Sadaka.”
8. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema kuwa:
“Enyi Waislamu! Je! niwaambieni mambo matano ambayo kwa hakika ni mema, maneno hayo yanawapelekeni hadi Jannat?
Ma-Sahabah wakajibu,
“Naam, lazima tuambie ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Naomba utuongoze.”
Kwa hayo Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. akasema:
“Mnapopatwa na misiba basi lazima mfanye subira na mujaribu kuficha, mutoe Sadaka kiasi kwamba mkono wa kulia unapotoa mkono wa kushoto usipate habari, muwatende mema wazazi wenu, na kwa hakika katika mambo hayo ndiyo kuna furaha ya Allah swt na kila mara mwezavyo kusema semeni, La Haula wala Quwwata illa billahil ‘Alliyyil ‘Adhiim, kwa hakika hiyo ni hazina moja kubwa katika hazina za Jannat, na vile vile katika nyoyo zenu muwe na mapenzi ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. pamoja na Ahlul Bayt a.s.