read

15. Fadhila za Kutoa Sadaka Katika Siku Tukufu

Mujipatie fadhila kwa kutoa sadaka katika siku tukufu na mwezi wa Ramadhani.

1. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:
“Kutoa Sadaka siku ya Ijumaa kuna thawabu na fadhila kubwa sana.”

2. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema:
“Msimkatalie masikini anayeomba siku ya ‘Arafah. Lazima mpeni chochote kile.”

3. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:
“Mtu yeyote atakaye kuwa ametoa Sadaka katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, basi yeye atakuwa ameepukana na balaa za aina sabini.”