read

19. Aina za Sadaka

1. Mu’alla bin Khunais amesema kuwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alikwenda katika makazi ya Banu Sa’id na wale wote waliokuwa na shida aliwawekea mikate na kuondoka zake. Hapo mimi nilimwuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s.:
Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimjibu :
“La! Hawa kama wangekuwa marafiki na wapenzi wetu na wafuasi wetu basi ningewaongezea kiasi cha punje ya chumvi”. 1

Hapo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliponielezea kwa uwazi zaidi kwamba siku moja Mtume ‘Isa bin Maryam a.s. alikuwa akipita ufuoni mwa bahari, na akatoa mkate kidogo kutoka kifurushi chake akatupa baharini. Baadhi ya wale aliokuwa nao wakamwuliza!
“Ewe Mtume Isa bin Maryam! Je! umefanya nini bwana? Nini maana ya kutupa mikate baharini?

Mtume Isa a.s akawajibu:
“Katika bahari kuna viumbe vya Allah swt na iwapo kutatokezea na viumbe vyovyote vitakavyo kula humo kutokana na nilichowatupia basi kwa hakika katika ufalme wa Allah swt nitakuwa na thawabu nyingi mno.”

2. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema:
“Pozeni nyoyo zenu kwa sababu ya kiu kali kwani Allah swt hupendezewa sana na tendo hilo. Kwa hakika amebahatika yule mtu ambaye anawamalizia kiu wanyama kwani yeye siku ya Qiyamah atapata msaada mkubwa sana atakapokuwa katika hali ya kiu.”

3. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alikuwa akifunga safari baina ya Makkah na Madina, akaona kuwa kulikuwa na mtu mmoja aliyejitupa chini ya mti mmoja. Basi Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamwamwambia mtu mmoja aliyekuwa naye, aende akamwulize hali yake, inawezekana labda alikuwa na kiu kali. Mtu huyo alipomwendea huyo mtu aliyekuwa amelala chini ya mti na kumwuliza hali yake basi ikajulikana kuwa mtu huyo alikuwa na kiu ya maji. Basi Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimnywesha maji na akaondoka kuendelea na safari yao. Yule aliyekuwa naye safarini akasema,
“Ewe mwana wa Mtume wa Allah! Huyu mtu alikuwa ni Mnasara, watu kama hawa pia tunaweza kuwasaidia na kuwapa Sadaka?”

Basi Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamjibu
“Naam ! Katika mazingira kama haya inawezekana.”

4. Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. alikuwa pamoja na wafuasi wake katika safari, na waliketi kwa ajili ya kula chakula. Na akatokezea Swala mmoja ambaye alikuwa akitafuta chakula, Imam a.s. akamwambia huyo
‘Swala njoo karibu, njoo ule nasi! Usiwe na wasiwasi utulie na ujue hapa kwetu hautakuwa na hofu yoyote, upo katika usalama.”
Kwa kusikia hayo Swala huyo alimsogelea Imam a.s. na alikula pamoja nao.

5. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema kuwa siku moja baba yake alikuwa pamoja na wenzake katika bustani yake na walipoketi kula chakula na mara akatokezea Swala mmoja aliyekaribia.

Hapo Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. . ambaye ni baba yake na Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. akasema:
“Ewe Swala, jina langu mimi ni (Imam) Zaynul 'Aabediin bin Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib a.s. na mama yangu Bi Fatima az-Zahra a.s., njoo ushiriki nasi katika kula. Na Allah swt kiasi alichokuwa amemjaalia cha chakula huyo Swala alikula.”

6. Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:
“Hakuna mtu yeyote mwingine isipokuwa ni Mwislamu tu anayeweza kuchinja wanyama wenu wa dhabihu siku ya Iddi na unapotoa Sadaka kutoka humo, lazima wapewe Waislamu tu. Na unapotoa Sadaka katika mali zinginezo unaweza kuwapa Kafir Zimmi ambao wenye kuhitaji misaada hiyo.”

  • 1. Yaani Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alikuwa anamaanisha hapa kuwa angewaongezea kidogo.