read

26. Kusaidia Kuwafikishia Sadaka Wanao Hitaji ni Sunnah

1. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:
“Iwapo mtu atapewa msaada ikapitia mikono themanini hadi ikamfikia aliyemustahiki basi kila mkono utapata haki sawa sawa ya malipo.”

Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Bora ya sadaka zote ni ile ambayo binaadamu baada ya kujitimizia mahitaji yake kwa moyo mkunjufu anatoa sadaka.”

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Yule atakaye fikisha msaada katika hali nzuri kwa mwenye kustahiki basi huyo mfikishaji wa sadaka atapata thawabu sawa kama za yule atakaye toa sadaka yake – hata kama katika kufikisha msaada huo kwa anayestahiki itachukua mikono elfu arobaini basi wote watapata malipo sawa kabisa kwani Allah swt hana upungufu wala kasoro ya aina yoyote ile, na wale watu wanaofanya Taqwa na kutenda mema basi laiti kama mngeweza kuelewa uhakika wa swala hili.”

4. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:
“Watoaji ni wa aina tatu
    • kwanza ni Allah swt mwenyewe ambaye anatoa kwa ajili ya malimwengu zote.

    • Pili ni yule mwenye mali na

    • tatu ni yule msaada unaopitishwa katika mikono yake au ni mtu ambaye anafikisha misaada hiyo.”

Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amenakiliwa riwaya na Abu Basir kuwa amesema:

“Watoaji ni wa aina tatu wa
    • kwanza kabisa ni Allah swt,

    • wa pili ni yule ambaye anatoa kutoka mali yake na

    • wa tatu ni yule anayefikisha kama msaidizi katika kufikisha msaada huo kwa mustahiki.”