read

27. Kumsaidia Mu’umin ni Sunnah

Kutoa katika mali yako kwa ajili ya kumsaidia mu’umin ni sunnah.

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Allah swt amefaradhisha kwa waja wake kwa kusisitiza kuwa kama yafuatavyo,
    • kwanza uadilifu na mapenzi yake pamoja na mu’min mwenzake kama vile ajipendeavyo yeye kwa ajili yake ndivyo ampendee mu’min mwenzake.

    • pili awe ameweka hisa fulani au kiasi fulani katika mali yake kwa ajili ya kutaka kumsaidia mu’min ndugu mwenzake. Na

    • tatu kumukumbuka Allah swt katika kila hali na hapa haimaanishi kuwa kwa kumsifu Allah swt peke yake au kwa kutoa uradi (tasbihi) bali hapa kuna maanisha ya kuwa kufanywe kwa kimatendo kabisa yale yaliyoelezwa katika dini yakiwa ni sehemu ya imani ya mtu.”

2. Aban ibn Taghlib anasema kuwa Siku moja yeye alimwomba Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amwelezee haki za mu’min mmoja juu ya mu’min mwingine. Kwa hayo Imam a.s. alimjibu:
“Ewe Aban! Achana nayo, usini shurutishe kukujibu ulicho uliza.”

Nami nikamwambia :
“Ewe Mola wangu niwe fidia kwako.”

Na baada ya hapo niliendelea kumsisitiza Imam a.s. anielezee na ndipo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alipoanza kuniambia :
“Haki ya mu’min mwenzako juu yako ni kwamba nusu ya mali yako iwe ni mali yake.”
Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akagundua kuwa rangi ya sura yangu imebadilika na akaniambia,
“Ewe Aban Je! huna habari kuwa Allah swt ameelezea habari za wale watu ambao wamezipenda nafsi za watu wengine kuliko hata nafsi zao?”

Nami nikamujibu: “Bila shaka, niwe fidia juu yako.”

Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akaendelea kujibu,
“Kwa hivyo nyie toeni nusu ya mali yenu muwape ndugu zenu mu’min, na kwa hayo pia haita maanisha kuwa nyie mmethibitisha mapenzi yenu kikamilifu, kwa sababu bado mko mnalingana. Kujitolea mhanga na kufikia kiwango hicho itathibitika pale ambapo hata katika nusu ya mali mliyobakia nayo mkatoa mkawagawia mu’min ndugu zenu.”

3. Muhammad bin Ajlan anasema kuwa yeye alikuwa pamoja na Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. na mara akatokezea mtu mbele yao akatoa salamu, na Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamwuliza
“Je! ndugu uliowaacha huko nyuma hali zao zikoje?”

Basi huyo aliyekuja akawasifu na akatoa sifa zao na akaelezea kuhusu hali zao zilivyokuwa. Kwa hayo Imam a.s. akauliza :
“Je! matajiri miongoni mwao wanawatunzaje wagonjwa wao?”

Basi huyo mtu akajibu :
“Ewe mwana wa Mtume wa Allah! Kidogo tu.”

Na Imam a.s. akamwuliza:
“Je! hao matajiri wanaonana mara ngapi na masikini?

Basi huyo mtu akajibu :“Mara chache tu.”

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamwuliza:
“Je! hao matajiri wanawasaidia kwa mikono yao hao masikini?

Kwa hayo huyo mtu akasema: “Ewe Mawla! Wewe unaniuliza mambo ambayo katika utamaduni wetu upo mchache sana.”

Kwa hayo Imam a.s. alimjibu,
“Je! wao watajidhaniaJe! kuwa wao ni Mashi’a wetu?”

Abu Ismail anasema kuwa:Yeye alimwambia Al Imam Muhammad al-Baqir a.s.,

“Ewe Maula niwe fidia juu yako! Kwa sasa hivi huko kuna Mashi’a wengi.”

Kwa hayo Imam a.s. akajibu:
“Je! wanawasaidia na kuwahurumia mafakiri na wenye shida? Je! wale wanao watendea mabaya yaani watu hao wema waliofanyiwa mabaya wanawasamehe hao wabaya walio watendea mabaya? Je! wanasaidiana miongoni mwao katika kamari ? 1

Kwa hayo yote mimi nikajibu :“Hapana sivyo hivyo.”

Hapo Imam a.s. akasema :
“Kwa hakika hao sio Mashi’a wetu. Basi mjue wazi kuwa Mashi’a wetu mienendo yao na desturi na utamaduni wao ni kama vile nilivyoelezea hapo.”

5. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. siku moja alimwuliza Sa’id bin Hasan:
“Je! inawezekana miongoni mwenu kuwa mu’min mmoja akatia mkono katika mfukoni mwa mu’min wa pili na akajitolea kiasi cha fedha alizo na shida nazo bila ya kusita au kuogopa na mu’min yule aliyetiliwa mkono mfukoni mwake asimzuie?”

Said bin Hasan akamjibu:
“Ewe Mawla! Kwa hakika mimi sina habari na jambo kama hili.”

Kwa hayo Imam a.s. akamwambia, “Kwa hakika hakuna chochote.”

Hapo mimi nikamwambia Imam a.s. :
“Je! hii inamaanisha kuwa sisi tumesha teketea na kuangamia?”

Imam a.s. kwa hayo akamjibu :
“Sivyo hivyo, miongoni mwenu udugu na upendo bado haujaingia nafsini mwenu.”

Na katika maswala ya dua imesha zungumziwa hadithi moja ambamo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema zipo aina tatu za dua ambazo kwa kufika kwa Allah swt hakuna mtu anayeweza kuzizuia. Miongoni mwake moja ni-
dua ya mu’min anayemwombea mu’min mwenzake na ambaye ametoa msaada kutoka mali yake kwa ajili ya ridhaa ya Allah swt na Ma’asumiin a.s. na
pili ni, dua kwa ajili ya mu’min mwenzake ambaye pamoja na uwezo wake anaomba hivyo na ambaye baada ya kujua shida na dhiki kali ya mu’min mwenzake hakuipuuzia bali amemsaidia.”

  • 1. Nimekitarjumu kitabu juu ya kamari : Katika Islam Uharamisho wa Kamari. Na kimechapwa na Bilal Muslim Mission of Tanzania, DSM, Box 200333