read

29. Sadaka Itolewayo Kwanza Inakwenda Katika Mikono ya Allah Swt

Ni sunnah kuubusu mkono wako mwenyewe baada ya kutoa sadaka na kukinusa kitu na kukibusu kitu ambacho unakitolea sadaka.

Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s. Amenakiliwa hadithi yake moja

isemayo kuwa:
“Wakati muwapapo sadaka masikini muwaombe wawaombeeni dua, na akaendelea kusema, baadaye kuubusu mkono wa yule uliyemsaidia (uliyempa sadaka) kwa sababu sadaka unayoitoa kwanza inakwenda katika mikono ya Allah swt ndipo inapoingia katika mikono ya mwombaji.

Kama vile Allah swt anavyosema katika Qur’an Tukufu, Surah Tawba, 9, Ayah 104:
‘Je! hawajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anapokea toba ya waja wake, na anazikubali sadaqah, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kupokea toba na Mwenye kurehemu?’

Ahmad bin Fahad anaandika katika kitabu chake kuwa:

“ Al Imam Zaynul 'Abediin bin Hussein bin 'Ali bin Abi Talib a.s. wakati wa kutoa sadaka alikuwa akiubusu mkono wake mwenyewe, na mtu mmoja alimwuuliza sababu ya kufanya hivyo na Al Imam Zaynul 'Abediin bin Hussein bin 'Ali bin Abi Talib a.s. alimjibu,
“Kwa sababu kufanya hivyo ni kwamba sadaka kwanza inakwenda katika mkono wa Allah swt ndipo baadaye huishia katika mkono wa mwombaji.”

3. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:
“Sadaka inayotolewa na muumin kwa hakika inafika mikononi mwa Allah swt na baadaye ndio anapewa aliye mwombaji. Na akaendelea kuelezea ayah ya Qur’an Tukufu, Surah Tawba, 9, Ayah 104:

‘Je! hawajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anapokea toba ya waja wake, na anazikubali sadaqah, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kupokea toba na Mwenye kurehemu?’

Jabir Al J’ufi amenakili riwaya kutoka Al Imam Muhammad al-

Baqir a.s. kuwa Al Imam Amir al-Mu’miniin ‘Ali bin Abi Talib a.s. amesema kuwa:
“Siku moja nilitoa sadaka ya Dinar moja, hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akaniambia,
“Je! unajua sadaka inapotolewa na mkono wa mu’min kabla yake yeye anakuwa amejitoa nje ya mitego ya masheitani sabini? Na kabla ya yule mwombaji hajapokea hiyo sadaka inakwenda katika mikono ya Allah swt?

Allah swt anatuambia katika Qur’an Tukufu, Surah Tawba, 9, Ayah 104:
‘Je! hawajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anapokea toba ya waja wake, na anazikubali sadaqah, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kupokea toba na Mwenye kurehemu?’

Mu’alla bin Khunais ananakili riwaya moja kutoka Al Imam Ja'afer

as-Sadiq a.s. kuwa amesema:
“Kila kitu Allah swt amekiwekea mtunza hesabu wake, isipokuwa sadaka tu, kwamba yeye ndiye mwenyewe anayeishughulikia. Na baba yangu a.s. alipokuwa akimpa masikini au mwombaji sadaka yoyote, alikuwa akiichukua tena akawa akiinusa na kuibusu na tena alikuwa akimrudishia mwombaji mikononi mwake kwa heshima na adabu.

Kwa sababu sadaka anayopewa mwombaji kwanza inakuwa imepitia katika mikono ya Allah swt ndipo inapoishia katika mikono ya yule anayeomba. Kwa hiyo mimi pia nimependelea kukibusu kitu kile ambacho kimeshaingia katika mikono ya Allah swt ndipo kikaenda katika mkono wa mwombaji!”

6. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:
“Kwa kila kitu isipokuwa sadaka tu Allah swt amemweka Malaika kutunza habari zake – na sadaka ameiweka katika usimamizi wake mwenyewe.”

Muhammad bin Muslim ameripoti riwaya moja ama kutokea

Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. au Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa:
“Al Imam Zaynul 'Abediin bin Hussein bin 'Ali bin Abi Talib a.s. kila alipokuwa akimpatia sadaka mwombaji basi alikuwa akiibusu mikono ya mwombaji huyo. Na alitokezea mtu akauliza sababu ya kufanya hivyo naye akajibu kwa sababu inatoka kwenye mikono ya Allah swt na inaingia katika mikono ya mwanadamu huyo mwombaji.”