30. Ni Sunnah Kukopa
Katika kutoa sadaka ni sunnah kukopa na kumlipa maradufu aliyekukopa wakati wa kutoa sadaka.
1. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. siku moja aliijiwa na mtu mmoja ambaye akasema:
“Je! kuna yeyote yule atakayeweza kunisaidia kwa kunikopesha? Mmoja katika Ma-Ansaar akainuka na kusema :
‘Ewe Mtume wa Allah ! Mimi nina uwezo wa kumkopesha”.
Basi kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamwambia:
“Mpe mifuko minne ya tende huyu mwombaji. Kwa kusikia hayo, huyo Ansaar akampa mwombaji kama vile Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alivyomwagiza”.
Baada ya kupita muda, huyo Ansaar alimwijia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kwa kufanya madai ya mifuko minne ya tende aliyokuwa amemkopesha Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ambayo Mtume alimpa mtu sadaka, basi Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamwambia Inshaallah basi nitakutimizia. Na ikafika mara tatu huyu mtu akawa anakuja kuomba alipwe deni lake na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kila mara alikuwa akimwambia Inshaallah nitafanikisha tu.
Mwishoni huyo mtu akashindwa kusubiri na katika hali hiyo akasema,
“Ewe Mtume wa Allah swt! Inshaallah, nimeisikia mara nyingi vya kutosha!”
Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akacheka na kuwageukia na Ma-Sahaba na kuwauliza,
“Je! kuna yeyote miongoni mwenu ambaye anaweza kunikopesha?”
Basi mtu mmoja akainuka na kusema,
“Ewe Mtume wa Allah swt! Naomba ukope kwangu”
Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kwa hayo akamwambia
“Je! una kiasi gani?”
Na huyu katika kumjibu akamwambia
“Kiasi chochote utakachokihitaji wewe.”
Hapo ndipo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamwambia
“Mpe mifuko minane huyu Ansaari.”
Huyo Ansaar akasema,
“Ewe Mtume wa Allah swt! Mimi nilikukopa mifuko minne tu, sasa kwa nini unanirudishia mifuko minane?”
Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamjibu,
“Mifuko minne ninakulipa na mifuko minne zaidi ninakuongezea zawadi kwa ajili yako.”
2. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema :
“Kwa hakika sadaka inayotolewa kwa moyo mkunjufu inalipia deni, na inaleta mfululizo wa baraka.”