read

31. Ni Haramu Kuomba Kama Hakuna Haja

1. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:
“Mtu yeyote atakayeomba chochote bila ya kuwa na dharura yake, basi Allah swt atamfanya awe muhtaji kwa maswala hayo kabla ya kufa kwake, na kwa sababu ya kuomba kwake huku kusikostahiki, yeye ataadhibiwa na kutupwa Jahannam 1.”

2. Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:
“Allah swt amekula kiapo kuwa mtu yeyote bila ya kuwa na shida au dharura kama atamwomba mtu amsaidie, basi kuomba kwake huko kutamfanya yeye lazima siku moja awe mwombaji.”

3. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alikuwa akisema:
“Enyi watu mfuate na kutekeleza nasiha za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., kama alivyosema:
“Iwapo mtu yeyote atajifungulia milango ya kuomba, basi Allah swt atamfungulia milango ya ufukara na umaskini.”

4. Muhammad ibn Muslim ananakili riwaya kutoka kwa Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. kuwa amesema:
“Ewe Muhammad! Iwapo waombaji wangelielewa mabaya katika kuomba, basi kamwe wasingeweka mikono yao mbele ya wengine; na iwapo mtoaji angezijua faida na mema basi kamwe asingeuzuia mkono wake katika kutoa sadaka na misaada. Na vile vile Imam a.s. akaendelea kusema, bila shaka yule ambaye ana mali na uwezo na huku anaendelea kuwa mwombaji basi siku ya Qiyama atafika mbele ya Allah swt huku uso wake ukiwa umejeruhiwa.”

5. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:
“Mtu yeyote ambaye ana maslahi ya vyakula vya kujitosheleza kwa muda wa siku tatu na pamoja na hayo anaendelea kuomba basi mtu huyo siku ya Qiyama atakuja mbele ya Allah swt huku uso wake utakuwa hauna nyama.”

6. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:
“Bila ya kuwa na dhiki na shida mwenye kula kwa kuomba basi ni sawa na mtu anayekunywa pombe.”

7. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema:
“Mimi kwa kiapo cha Allah swt ninasema kuwa ni ukweli kabisa kuwa yeyote atakayeilisha nafsi yake kwa kujifungulia milango ya kuomba, basi Allah swt lazima atamfungulia milango ya ufukara na umaskini.”

8. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:
“Mtu yeyote anayejifungulia mlango wa kuomba, wakati anao uwezo wa kujilisha mwenyewe basi Allah swt atamfungulia milango sabini ya ufukara na umaskini, kiasi kwamba hakuna yeyote atakayeweza kuufunga hata mlango wake mdogo kabisa.”

9. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:
“Mtu yeyote ambaye ataunyoosha mkono wake kwa kuomba huku ana chakujitosheleza kwa siku moja pia, basi huyo mtu atahesabiwa miongoni mwa wafujaji.”

10. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:
“Siku ya Qiyama Allah swt hatawaangalia watu wa aina tatu na wala hatawatakasisha na watu kama hawa watapewa adhabu kali kabisa.
Kwanza ni mwanaume yule ambaye anafanya ulawiti,

mwanamke yule ambaye hakubakia na haya yoyote na

tatu ambaye pamoja na kuwa na mali bado anaendelea kuomba kwa watu.”

  • 1. Nimekitarjumu kitabu juu ya Jannat (Peponi ) na Jahannam (Motoni)