34. Uombaji
• Mufadh-dhal bin Kais bin Rumman anasema kuwa:
“Yeye siku moja alikuwa katika huduma ya Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., na mimi nikamdokezea kidogo kuhusu matatizo niliyokuwa nayo. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamwambia kijakazi wake:
Naomba ule mfuko. Na akaniambia Abu Ja’afar (Manthur) amenitumia hizi Dinar mia nne kwa ajili ya msaada, hivyo chukua wewe. Na uende ukamalize shida na dhiki uliyo nayo.”
Nami nikamwambia:
“Hapana! Kwa kiapo cha Allah swt mimi niwe fidia juu yako - mimi sina nia hivyo – mimi nilikuwa natarajia kuwa wewe uniombee dua kwa Allah swt ili shida na dhiki niliyonayo isiwe ngumu bali iwe nyepesi.”
Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akasema,
“Pamoja na mimi kukuombea dua, kamwe usiwaambie mbele ya umati wa watu shida zako kwani kwa kufanya hivyo wewe utapoteza heshima na hadhi yako.”
• Harith Hamdani anasema kuwa yeye amesikia hadithi ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kutokea kwa Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s. kuwa:
“Maombi ni amana za Allah swt katika vifua vya watu na yeyote yule atakayeficha siri hiyo basi atapata thawabu za ibada.”
• Kulayni anasema kuwa Bwana Luqman alikuwa akimpa mafunzo mwanawe kwa kumwambia:
“Ewe mwanangu, mimi nimesha kunywa dawa na magamba yaliyo chungu kabisa, lakini mbele ya shida na dhiki hakuna kitu kinachozidi uchungu wake. Iwapo wewe utapitia katika hali kama hiyo, basi kamwe usiseme maombi yako mbele ya watu, kwa sababu wewe katika macho yao utaanguka heshima na taadhima yako, na watu hao hawawezi kukufaidisha chochote na badala yake nakuomba umwombe yule ambaye anakujaribu kwa mitihani ya aina hiyo, na bila shaka ni yeye tu anayeweza kukuondolea matatizo na dhiki iliyokukabili, hivyo umwombe yeye tu (Allah swt). Yeye ni nani duniani ambaye amemwomba Allah swt na akarudi mikono mitupu, na yupo ambaye aliweka matarajio na matumaini yake kwa Allah swt na akajikuta ametoka mtupu?”
• Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. anaripotiwa kuwa amesema:
“Ewe 'Ali! Allah swt ameweka amana miongoni mwa waja wake katika hali ya shida na ufukara, na yeyote yule atakayeweza kuificha hiyo amana basi ajue kuwa yeye ni mtu ambaye amedumisha ‘ibada na anapata fadhila za wale walio dumisha ‘ibada na wanao funga saumu, lakini yeyote yule ambaye anaitoboa na kuitangaza hiyo amana ya Allah swt kwa kudhihirisha na kufanya bayana siri ya shida na ufukara wake kwa wengine, na hao watu baada ya kumsikiliza hawamsaidii basi mjue kuwa huyo mtu kwa hakika wamemuua. Mauaji haya sio kwa upanga au kwa mkuki bali ameuawa kimoyo.”
• Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripoti riwaya kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa amesema:
“Enyi wenye shida na masikini! Tunzeni heshima zenu na mpeni Allah swt furaha ya mioyo zenu ili kwamba Allah swt awalipe mema kwa ufukara na shida zinazo wakabili na kama nyie hamtafanya (isije mkakufuru na kuvuka mipaka kwa sababu ya kukosa subira na hekima) hivyo basi mtambue kuwa mtapata adhabu na gadhabu za Allah swt.”