35. Ruhusa Kumwambia Shida Zako Mu’umin
Kuruhusiwa kumwambia shida zako mu’umin na ndugu pale inapotokea.
• Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakiliwa katika riwaya moja amesema kuwa:
“Itakapo tokea miongoni mwenu mtu akazingirwa kabisa kwa hali mbaya, basi inambidi awajulishe jamaa na ndugu zake na asiiweke nafsi yake katika shida.”
2. Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s. amesema katika Nahjul Balagha kuwa:
“Mtu yeyote atakayemwambia mahitaji yake dharura zake kwa muumin basi ajue kuwa ameweka habari zake hizo kwa Allah swt, na yeyote yule atakayeleta dharura na mahitajio yake kwa kafiri basi ajue kuwa amekwenda kinyume na maamrisho ya Allah swt.”
• Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:
“Katika hali tatu tu ndipo kunapo ruhusiwa kuomba ama sivyo hairuhusiwi.
Kwanza katika kujinusuru mtu mwenyewe,
Pili, kujinusuru na hasara kubwa kabisa ya mali na
tatu iwapo kwa kutokuomba kutakuja kumpatia udhalilisho wa hali ya juu sana. Yaani mtu katika vitu hivyo vitatu, kujiokoa na hali hizo tatu mtu anaweza kuomba msaada kwa wengine.”
4. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema kuwa:
“Mtu mmoja alimwijia Al Imam Hasan ibn 'Ali bin Abi Talib a.s. na kuomba chochote Kwa hayo Imam a.s. akamwambia haistahiki kuomba isipokuwepo hizo sura tatu.
Kwanza ama kuzuia umwagikaji wa damu,
ama mtu akiwa na shida ya hali ya juu kabisa au
kujizuia kuja kudhalilika vibaya sana.
Sasa hebu wewe niambie wewe upo katika sura ipi kati ya hizi tatu?
Yeye akasema ‘Ewe mwana wa Mtume wa Allah! Katika sura tatu ulizozitaja ipo mojawapo. Basi bila kusita kwa haraka sana Al Imam Hasan ibn 'Ali bin Abi Talib a.s. akamtolea dinar elfu hamsini na kumpa, na Al Imam Hussein ibn 'Ali bin Abi Talib a.s. akampa dinar elfu arobaini na tisa na ‘Abdulah bin Ja’afar akampa dinar elfu arobaini na nane.”