37. Namna Amali Njema ya ‘Kusaidia’ Inaweza Kuharibika
Si vyema kumsema mtu baada ya kumsaidia au kumsema yule uliyempa sadaka.
• Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa akisema:
“Allah swt amechukia na hafurahishwi na sifa sita na vile vile mimi sizifurahii hizo sifa sita na ndio nimefanya usia kwa mawasii na wafuasi waumini wote kuwa vitu hivyo sita wajiepushe navyo na mojawapo ni kule baada ya kutoa sadaka mtu akaanza kumsema yule aliyepokea (hiyo sadaka).
2. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:
“Baada ya kutenda mema mtu atakapovizungumzia hayo basi atayateketeza mema yake yote.”
3. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili riwaya kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa:
“Allah swt hakupendezewa na mambo sita na mimi vile vile katika kizazi change, Maimamu wote sikupenda kutokezee sifa hizo, na vile vile Maimamu pia nimewausia kuwa wasizipende sifa hizo ziwepo katika muumin. Hivyo kila muumin anabidi ajiepushe na sifa hizo. Katika sifa hizo sita mojawapo ni ile baada ya kumfanyia mtu wema mtu anaanza kuyazungumzia huku na pale.”
4. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. anasema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:
“Allah swt hapendi sifa sita na hizo sifa sita mimi sikupendezewa kwa ajili ya mawasii watakaonifuata na waumini wote watakaonifuatia.
• Kwanza kusali isivyo- bila makini (kutikisika mikono au kukunakuna katika sala)
• pili katika hali ya saumu kujamiiana na mwanamke
• tatu baada ya kutoa sadaka kutangaza na kuonyesha
• nne kuingia msikitini katika hali ya Janaba
• tano kuwa na shauku ya kutaka kujua mambo ya watu, majumbani mwao kunatendeka na kunaendelea nini, na
• sita kucheka makaburini mtu anapokuwa baina ya makaburi mawili.”
5. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kwa mamlaka yake amenakili riwaya kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa:
“Mtu yeyote atakaye msaidia muumin ndugu yake na baadaye akaja akamwambia kuhusu wema huo akausema basi Allah swt hulirudisha tendo hilo halikubalii. Basi mtoaji atabakia na uzito juu yake na kwa lile jema alilolitenda hana malipo yoyote kutoka kwa Allah swt.”
Na Imam a.s. aliendelea kusema: “Kwa sababu Allah swt anasema kuwa yeye ameiharamisha Jannat kwa ajili ya yule anayesema baada ya kutenda tendo jema na bahili na mchonganishi.
Muelewe wazi kuwa yule mtoa sadaka, hata anayetoa kiasi cha Dirham moja, basi Allah swt humlipa zaidi ya ukubwa wa mlima wa Uhud kwa neema za Jannat na yeyote yule atakaye saidia kufikisha hiyo sadaka kwa yule ambaye anahitaji basi Allah swt atamlipa mema hayo hayo, na kamwe hakutakuwa na punguzo lolote katika neema za Allah swt kwa ajili ya wote hao.”
6. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika hotuba yake alisema:
“Yeyote yule atakaye tenda wema na kuwawia wema ndugu wenzake, na akaanza kutanganza mema aliyoyafanya basi matendo ya watu kama hawa yatatupiliwa mbali na hayatakuwa na maana yeyote.
Allah swt amewaharamishia Jannat watu wafuatao:
• Kwanza ni wale wanao tangaza mema waliyowafanyia watu wenzao, na
• Wale wanaowapotosha watu wengine,
• wafitini,
• wanywaji wa pombe,
• wale wanao tafuta makosa ya watu na aibu za watu,
• wale wenye tabia mbaya,
• wale walio makatili kwa wenzao na vile vile
• wale watu wanao watuhumu watu wengine kwa tuhuma za kuwazushia maovu.”
7. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili riwaya kutoka kwa mababu zake kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:
“Allah swt amewazuieni nyinyi kwa matendo maovu takriban ishirini na manne na mojawapo ni jambo lile ambalo baada ya kutoa sadaka mtoaji anamwambia maneno aliyempatia.”
8. Bwana Abu Dhar Al-Ghafari amenakili riwaya kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa:
“Kuna aina tatu ya watu ambao Allah swt kamwe hatazungumza nao siku ya Qiyama.
• Kwanza ni yule mtu ambaye hatoi kitu chochote bila ya kumsema au kumwambia yule anayempa, na
• pili ni yule ambaye hachukui jukumu wala haoni umuhimu wa kuficha sehemu zake za siri na wa
• tatu ni yule ambaye anauza mali yake na kutaka faida kupindukia kiasi.”
9. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:
“Mtu yeyote baada ya kumsaidia muumin atamuudhi kwa kumwambia au kwa kumsengenya kiasi kwamba roho yake ikaumia basi Allah swt huibatilisha sadaka na wema kama huo.”
10. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:
“Aina tatu ya watu kamwe hawataingia Jannat.
• Moja ni mtu yule ambaye wazazi wake wamemfanya Aak, wa
• pili ni mnywaji wa pombe (daima anakunywa pombe) na
• tatu ni yule baada ya kufanya mema huanza kusema na kutangaza.”