38. Si Haki Kuwa Mwenye Shida Asipoomba Basi Asisaidiwe
Mtu anapotoa kitu kusaidia basi hairuhusiwi kumwambia kuwa umetoa zaidi kupita kiasi.
Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:
Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s. siku moja alimtumia mifuko mitano za Tende za Baqi’ (Jannatul Baqi’, ipo Madina). Mtu huyo alikuwa muhtaji mwenye shida na daima alikuwa akitegemea msaada kutoka kwa Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s., na kamwe alikuwa harefushi mikono yake kwa wengine kwa ajili ya kuomba kwa watu wengineo. Mtu mmoja alipoyaona hayo basi alimwambia Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s.:
“Kwa kiapo cha Allah swt, huyu mtu hajakuomba chochote wewe kwa hivyo badala ya kumpa mifuko mitano mfuko mmoja tu ulikuwa ukitosha, na kwa hayo Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s. akamwambia:
“Allah swt asiongezee idadi ya mu’min kama wewe humu duniani! Wewe mtu wa ajabu sana, mimi ndiye ninayempa lakini ubahili unaufanya wewe! Kumbuka kuwa mtu mwenye shida na anayekutegemea wewe hakuombi, Je! ni haki kuwa mwenye shida asipoomba basi asisaidiwe mpaka lazima aombe? Basi hapa inaonyesha heshima yake. Uso ule ambao unawekwa juu ya udongo kwa ajili ya ibada ya Allah swt katika hali ya sujudu itakuwa basi mimi nimeubadilisha ule sura badala ya kumwangukia Allah swt utakuwa umeniangukia mimi! Na jambo ambalo silitaki mimi na wala silifanyi hivyo.”
Mtu ambaye hathamini na hajali shida za waumini wengineo itakuwaje ategemee Jannat wakati huku yeye mwenyewe anafanya ubahili katika mali yake?
Yule asemaye daima “Ewe Allah swt wasamehe madhambi yao yote waume kwa wanawake Waislamu” kwa hakika mtu kama huyu huwa anategemea Jannat tu; Je! ni uadilifu gani kwa kusema tu kwa mdomo kuwaombea mema watu ambapo wao hawawafai watu wengine wanapokuwa na shida na dhiki huku wakiwa wanafanya ubahili kwa mali zao?”