48. Mtoe Sadaka Kutoka Vile Vitu Mnavyovipenda Sana
1. Al-Kulayni anaandika riwaya kuwa Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. :
“Ilikuwa ni tabia yake kuwa alikuwa kila alipokuwa akikaa kula alikuwa ana beseni moja ambamo alikuwa akiweka kila aina chakula iliyokuwa mbele yake kidogo kidogo na alikuwa akitoa hukumu kuwa beseni hiyo ipelekwe kugawiwa kwa wenye shida na muhitaji. Na hapo akasoma ayah ya Qur'an Tukufu ifuatayo: Surah Al Balad, 90, ayah 11:
“Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani.”
Na baadaye akasema Allah swt anaelewa wazi wazi kuwa (hakuna) katika uwezo wa kila mtu kumfanya huru mtumwa kwa hiyo na hivi ndivyo alivyofungua njia ya kumfikisha mtu hadi kuingia Jannat.”
2. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. katika Sadaka alizokuwa akitoa alikuwa akitoa sukari pia.
Kwa hivyo kulitokea mtu mmoja akamwuliza, Yabna Rasulallah! Kwa nini unatoa sukari?
Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alijibu:
“Mimi ninapenda sana sukari, na ninapenda kuwa niwe nikitoa Sadaka kwa kile kitu ninachokipenda sana katika njia ya Allah swt.”