49. Sadaka Mmoja Bora ni Kuutuliza Kiu cha Maji
Imesisitizwa mno kuwanywesha maji wanaadamu na wanyama hata kama hapo kutakuwa na maji mengi mno.
1. Al-Kulayni amemnakili Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ambaye naye amemnakili Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. riwaya kuwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:
“Siku ya Qiyama tendo jema kabisa malipo yake watapewa wale
watu ambao wamefanya wema katika kugawa maji.”
Riwaya hiyo hiyo Sheikh Saduq a.s. ameielezea pia.
2. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema: “Sadaka iliyo bora kabisa ni ile ya kuutuliza moyo unaowaka kwa kiu cha maji.”
3. Ali ibn Ibrahim amenakili riwaya kutoka kwa baba yake kuwa
Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:
“Pale panapokuwa na maji na mtu akatoa Sadaka ya kuwagawia watu maji basi Allah swt humjaalia thawabu za kumfanya huru mtumwa mmoja, na pale ambapo hakuna maji kabisa na mtu akatoa Sadaka ya kugawa maji basi Allah swt humhuisha mtu mmoja na kwa hakika mtu anayemhuisha mtu mmoja ni sawa sawa na kuhuisha ulimwengu mzima.”
Riwaya hii vile vile Sheikh as-Saduq ameinakili.
4. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema kuwa:
“Siku moja alikuja Mwarabu mmoja kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na kumwambia:
“Ewe Mtume wa Allah swt! Naomba unionyeshe tendo ambalo litaniingiza mimi peponi. Kwa kusikia hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akasema: Chukua Mashk (chombo cha kujazia maji iliyokuwa ikitumika katika zama hizo na ilikuwa ikitengenezwa kwa ngozi) na uwapelekee maji hayo familia ambayo ipo inateseka kwa kukosa maji na kiu kinawasumbua sana kiasi kwamba watakapo pata maji hayo watayanywa kwa haraka sana. Basi uelewe kuwa wewe utaipata Jannat kabla hata maji hayo hayajaisha au Mashk yako hiyo haijatoboka.”
5. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema:
“Bila shaka, Allah swt anafurahishwa mno kwa kuona mtu anawanywesha maji wanaadamu au wanyama ambao kwa joto au kiu kali kabisa kinacho wasumbua hao na Allah swt siku ya Qiyama atamjaalia kivuli. Na kwa hakika hakutakuwa na kivuli kingine chochote isipokuwa kile kilichotolewa na Allah swt tu.”
6. Ibn Abbas anasema kuwa mtu mmoja katika kutaka kumhurumia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akasema:
“Ewe Mtume wa Allah swt! Je! ni tendo gani lile nifanye mimi ili niweze kuwa mustahiki wa kuingia Jannat?”
Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamwambia:
“Nunua Mashk moja mpya na uwe ukiwanywesha watu maji kutoka humo, hadi Mashk yako hiyo itakapofika hatua ya kuja kutoboka (yaani itakapo chakaa au kuzeeka). Basi kwa tendo hili kwa hakika ndilo litakalo kufikisha wewe Jannat.”
7. Abu Hamza Thumali amenakili riwaya kutoka kwa Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. kuwa amesema:
“Yeyote yule atakaye mlisha na kumshibisha mu’min ambaye ana njaa basi Allah swt siku ya Qiyama atamlisha matunda ya Jannat, na yeyote yule atakaye tuliza kiu cha mu’min ambaye ana kiu basi Allah swt siku ya Qiyama atamnywesha maji ambayo yamepigwa lakiri. Na yeyote yule atakaye mvalisha mavazi nguo mu’min ambaye kwa hakika ana shida basi Allah swt siku ya Qiyama atamvalisha mavazi kijani ya Jannat.”