read

52. Kugawa Nusu ya Mali Katika Sadaka ni Sunnah

Halabi anasema kuwa yeye alipomwuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. basi Imam a.s. akamjibu:
“Naam kabisa! Al Imam Hasan ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. aligawa nusu ya mali yake katika njia ya Allah swt – hadi kwamba nguo kwa nguo, Dinar kwa Dinar, alivigawa vyote katika njia ya Allah swt, na alikwenda Hija ishirini kwa kutembea na miguu.”