7. Zaka Zilizo Sunnah
Vitu saba vina Zaka Sunnah:
1. Mali ya biashara au mtaji
Mali ambayo mtu anataka kuitumia katika kufanyia bishara
2. Aina za nafaka :
Mfano mchele, dengu, dengu iliyoparazwa. Lakini mbogamboga kama vile biringanya, matango, matikimaji, maboga hayana Zaka.
3. Farasi jike
4. Vito vya dhahabu na mawe
Vitu vilivyotengezwa vya kuvaa na mawe kama almasi n.k.
5. Mali iliyozikwa au kufichwa
Iwapo mtu atakuwa na mali aliyoizika au aliyoificha ambayo hawezi kuitumia basi kwa misingi ya uwezo inambidi kutoa Zaka ya mwaka mmoja.
6. Kukwepa kutoa Zaka
Iwapo mtu atauza sehemu ya mali kiasi fulani kabla ya kuisha kwa mwaka kwa misingi ya kukwepa kulipa Zaka, basi itambidi uanzapo mwaka mpya, alipie Zaka sehemu hiyo aliyokuwa ameuza kwa ajili ya kukwepa Zaka yake.
7. Mali ya kukodisha
Mtu anayepokea malipo kutokana na kukodisha majumba, maduka, mashamba, mabustani au hamaamk (mabafu yanayotoza malipo kwa kutumia).