read

Dibaji

Namshukuru Mwenyezi Mungu Mola wa watu wote, Rehma na amani zimshukie Hashima, yeye na ahli zake.

Utukufu wa Seyyidna Ali mbele ya Mwenyezi Mungu ni jambo lisilo na shaka. Amezaliwa na wazazi watukufu na akalelewa na mtukufu waviumbe ambaye ni mtume Muhammad (s.a.w.w).

Imam Ali bin Abi Talib alikuwa ni mwanafunzi wa kwanza wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Na ndiye wa mwanzo kumsadiki kwa kila jambo, hivyo yeye ndiye "Siddiqul-A’adham." Pamoja na yote hayo Seyyidna Ali cheo chake kwa Waislamu ni sawa na uzi unaodhibiti tasbihi, bila ya uzi huo, tasbihi lazima zitawanyike.

Kwa maana hii, kusoma na kujua maisha ya Seyyidna Ali ni jambo la wajibu lililo muhimu.

Namshukuru Maulana Seyyid Naqi Saheb kwa kututayarishia na kutueleza vyema maisha ya Imam Ali, ambaye ni kiungo muhimu katika Uislamu.

Hawakukosea wale wanaomwita Seyyidna Ali kuwa ni "Imamu-mashaarik wal-maghaarib", katika salaa za Ijumaa sifa hiyo ni yake hasa na haimfai yeyote katika sahaba za Mtukufu Mtume (s.a.w.w). Kitabu hiki kitasaidia vema katika kuwajumlisha Waislamu, kwa kuelewa maisha sahihi ya Imam Ali (Karamallahu Wajhahu).

Ni tumainio langu kuwa kitabu hiki mtakipenda.

Ahsanteni Ndugu yenu,

Muhammed Omar Ali,
S.L.P. 45920,
Dar es Salaam.