read

Sababu Za Uchelewesho Katika Uandishi Wa Hadith

Inafahamika vyema kabisa kuwa Mtume s.a.w.w., kuanzia mwanzoni kabisa mwa Utume wake, aliupatia umuhimu zaidi kuhusu uandishi wa Qur’an. Kimatokeo Qur’an ikawa ipo mbali na makosa au mabadiliko (tahrif). Hata hivyo, katika hali ya Hadith kwa mujibu wa imani yetu mbali na ruhusa au amri ya Mtume s.a.w.w. kwa kuhusiana na uandishi wa Hadith na mbali na ukweli kwamba Hadith zilikuwa zimeandikwa katika zama za uhai wa Mtume s.a.w.w., sio kwamba tu kuwa haukupewa umuhimu kwa kazi, pia iliweza hata kupingwa. Upingamizi huo ulisababisha matatizo mengi kuhusiana na Hadith, ambayo tutayaona hapo mbeleni.

Uchelewesho huo wa kuziandika Hadith na matokeo yenye hatari yalifanya kikundi kimoja kumtupia lawama na'udhubillah Mtume s.a.w.w. Wao walitambua wazi kuwa upingamizi wa uandishi wa Hadith iwapo itatokea kwa Mtume s.a.w.w., basi haitaweza kulaumiwa, kwani Mtume s.a.w.w. hawezi kulaumiwa; hata hivyo, iwapo wataielezea kwa wengine basi itatoboa udhaifu wao. Kwa hivyo, walimwelekezea Mtume s.a.w.w. kuwa ndiye aliyekataza kuandikwa kwa Hadith.

Riwaya Ya Abu Sa'id:
Riwaya ifuatayo imenakiliwa kwa mamlaka ya Abu Sa'id al-Khudhri:

"Musiandike chochote kile kutoka kwangu isipokuwa Qur’an tu, na yeyote yule aliyekwisha andika chochote kile basi ni lazima ayateketeze yote."1

Taarifa hiyo ni wazi na yenye maana isiyofahamika. Maana inayotakiwa kuelezwa ni kwamba hakuruhusiwi kuandikwa kwa Hadith. Kwa mujibu wake, mtu yeyote aliyekuwa ameandika chochote kile basi lazima akiteketeze. Ni sawa kabisa kwa sababu ya uwazi wa ubainishi wake, vile vile pamoja na sababu zinginezo, ndiyo maana sisi hatuwezi kuikubali uhakiki wa taarifa hiyo au nyinginezo kama hizo. Sababu zetu za kutokubaliana na Hadith hiyo ya juu ni kama zifuatazo:

Kwanza, iwapo sisi tutaikubalia Hadith hii basi hatuwezi kuifungia kipindi cha muda. Iwapo uandishi wa Hadith ulikatazwa na haram, basi ni haram katika kila zama. Hata hivyo, sisi twaona wanaoinakili Hadith hii, wao wenyewe hawakuifuatilia na wao hatimaye waliziandika na kuzikusanya Ahadith. Uandishi huu, kama ilivyoonekana hapo juu, ulianza katikati ya karne ya 2 A.H./8 A.D., na kukosekana kwa utiifu wa Hadith inatuonyesha kuwa hao wanainakili Hadith walikuwa hawakuichukulia kama sahihi na kweli; kwani hao walijua kuwa chochote kile kilichoharamishwa na Shariah haiwezi kubadilishwa kikawa halali. Jambo la kuvutia humu ni kwamba wao wameirekodi hata Hadith hii, ambavyo wao hawakuifuatilia, kwa kalamu zao zilizobarikiwa! Je, itawezekanaje sisi kuiamini kuwa ni sahihi na kweli?

Pili, waandishi hawa hawa pia wamezinakili Hadith zinginezo zinazozungumzia kuruhusiwa kuandikwa kwa Hadith,2 na iwapo sisi tutazichukulia Hadith zote mbili kuwa ni sawa katika maelezo na maelekezo, basi itatulazimu kuziachia mbali Hadith zote mbili hizo kwa sababu ya kupingana kwao kwenyewe. Kwa hivyo, katika hali kama hii Hadith hizi zote mbili zinapoteza ustahi wa kuaminika; navyo hata sisi, kwa kudhania tu, hatuwezi kamwe hata kutumia njia zinginezo kusadikisha Hadith ambayo ipo inakataza uandishi wa Hadith za Mtume s.a.w.w.

Tatu, Abu Sa'id al-Khudhri, ambaye anatajwa hapo juu kwa wingi katika kuinakili taarifa hiyo, pia anatoa taarifa nyingine inayopingana na ile ya kwanza, yeye anasema: "Katika siku hizo, sisi tulikuwa hatuandiki chochote kile isipokuwa Qur’an na tashahhud (ushahidi)." 3

Nukta mbili zinaweza kufahamika kwa kujua sababu zake kutokana na taarifa za Abu Sa'id. Kwanza, Abu Sa'id haelezi kuwa kutoandika kwao Hadith kulitokana na amri ya Mtume s.a.w.w. kwani kama ingalikuwapo, basi angalionyesha hayo, hadi hapo isemwe kuwa maelezo kama hayo hayakuazimiwa hapa. Uwezekano huu wa pili uliotolewa, ingawaje unaweza kuchukuliwa kwetu sisi, inaonekana ya mbali mno. Na nukta ya pili ni kuongezwa kwa neno tashahhud katika taarifa hii, kitu ambacho hakipatanishi pamoja na kusudi la uharamisho wa kuandika isipokuwa Qur’an tu. Ni jambo la kutilia maanani kwamba Hadith nyingine kutoka kwa Ibn Mas'ud, neno istikharah limeongezwa pamoja na tashahhud.4

Kwa kuhusiana na Hadith hii, inawezekana kukaulizwa, je, ni kwa nini Mtume s.a.w.w. aruhusu uandishi wa tashahhud pekee yake, ambapo inatambuliwa kuwa kutapotea vile wakati uendeleavyo, hayo pia yaliweza kutokea pamoja na Hadith zinginezo, baadhi yao ambazo zilikuwa na maongozo muhimu kabisa ya Shariah za Dini. Na katika upande wa pili, iwapo kulikuwapo na madhara yoyote katika kuziandika Hadith, basi madhara hayo pia yaliweza kutokezea katika kuandika tashahhud au chochote kile. Kwa hivyo, haikubaliki kimantiki kudai kuwa Mtume s.a.w.w. ndiye aliyeharamisha kuandikwa kwa Hadith.

Nne, kile kinachoweza kukusanywa kutokana na historia - ambacho sisi tutalisemea kwa zaidi hapo mbeleni - Abu Bakr, na hata Khalifa wa pili, walipendekeza kuandikwa kwa Hadith mwanzoni mwa Ukhalifa wao. Hata hivyo, hapo baadaye wao waliharamisha kwa kutolewa kwa sababu zao. Hao Makhalifa kamwe hawakusema kuwa kazi kama hiyo ilikuwa imeharamishwa na Mtume s.a.w.w. Zaidi ya hayo wao waliposhauriana na Sahaba wengineo kuhusu kuandika Hadith, nao pia walipendezewa na shauri hilo. Hii pia linatuthibitishia kuwa hapakutolewa amri na Mtume s.a.w.w. ya kuharamisha kuandika kwa Hadith.

Katika mojawapo ya Hadith Abu Basir anaripotiwa akiwa amemwambia Abu Sa'id al-Khudhri: "Sisi twaandika chochote kile tukisomacho." Abu Sa'id alimwambia: "Je, wataka kuyakusanya ili ukitengeneze Kitabu? Mtume s.a.w.w. ametuelezea Hadith nasi pia twakuambia wewe, nawe pia kama sisi ni lazima uzikariri tu kwa mdomo bila ya kuandika."5 Nukta mbili hapa zinastahili kuchunguzwa. Kwanza, Abu Sa'id hasemi kuwa Mtume s.a.w.w. ndiye aliyeharamisha uandikwaji wa Hadith. Pili, sababu aitoayo kwa kutoziandika Hadith ni sawa na zile zilizoripotiwa kutokea kwa Khalifa wa pili, ambaye naye pia hamsemi Mtume s.a.w.w. kuwa ndiye aliyeharamisha uandishi wa Hadith. Katika hali yoyote ile, ni jambo la kuyakinisha kuwa Mtume s.a.w.w. kamwe hakuharamisha uandishi wa Hadith.

Tano, kuna taarifa katika Hadith, moja kwa moja baada ya kutajwa hiyo ya juu, na kuwapo kwake pia kunatudalilishia kule kutothaminiwa kwake:
"Simulieni (chochote kile utakacho) kutokea Waisraili. Hakuna madhara ndani yake." Kuanzia mwanzoni kabisa, kwa upande mmoja Mtume s.a.w.w. anafahamika kwa kuchukizwa mno katika kusikia hadithi za Mayahudi (hujulikana kama Israiliyyat) - na kwa upande wa pili, Wanazuoni wa Kiislam wamekwisha zitambua madhara ya mawazo yanayoenezwa nayo, inaweza kusemwa kuwa Hadith hiyo nzima ni kazi ya uzushi mtupu. Hadith hii inawataka Waislam kwa upande mmoja, waziandike Hadith za Mtume s.a.w.w., na hatimaye kwamba zitaweza kusahauliwa pole pole; na upande wa pili, inawapatia leseni ya bure ya kuunganisha chochote kile wakitakacho kutoka kwa Mayahudi, Haya ndiyo maazimio maovu kabisa za Hadith kama hizi za kuzuliwa. Je, kunaweza mtu yeyote mwenye akili timamu akasema kuwa Mtume s.a.w.w. ndiye aliyetoa amri kama hiyo?

Sita, ipo Hadith nyingineyo kutokea Abu Sa'id al-Khudhri ambayo inatuletea uwezekano wa Mtume s.a.w.w. kutomruhusu Abu Sa'id kuandika Hadith kutokana na sababu maalum, ingawaje, katika mtazamo wetu, uwezekano wa kuruhusiwa katika swala hili pia ni kwamba Hadith hii vile vile ni uzushi. Abu Sa'id asema:"Mimi nilimwomba Mtume s.a.w.w. ruhusa ya kuandika Hadith, lakini yeye alikataa kunipa idhini." 6 Je kwa sababu zipi?

Hadith hii inatuunga mkono katika uwezekano wa Mtume s.a.w.w. kwa kumkatalia ruhusa ya kuandika Hadith katika swala la Abu Sa'id. Wakati inapozingatiwa katika nuru ya Hadith, ambazo sisi tutazinakili hapo mbeleni, ambapo Mtume s.a.w.w. yupo anaripotiwa kwa kutoa idhini kwa watu wengineo basi uwezekano huu utajipatia nguvu zaidi.

  • 1. Taqyid al-’ilm. uk. 29,31; Musnad Ahmad, vol. 3, uk.12,21,39; sunan al-Sarimi, vol. 1, uk 119.
  • 2. Jami’bayan al-ilm, vol. 1, uk.76; Kashf al-astar, vol. 1, uk 109.
  • 3. Taqyid al-ilm, uk. 93; al-Msannaf, ya Ibn Abi Shaybah, vol.1, uk.293.
  • 4. Al-Musannaf, ya Ibn Abi Shayban, vol. 1, uk.294.
  • 5. Taqyid al-ilkm, uk. 36,37.
  • 6. Taqyid al-ilm, uk.36.