Al-Qur’an Na Uandishi
Al-Khatib al-Baghdadi, ili kuunga mkono maelezo yake juu ya ruhusa ya uandikaji wa Hadith, anaelezea uthibitisho kutokea aya za Qur’an. Katika misingi ya Qur’an inayotuamrisha kuandika vyote vile ambavyo vina hatari ya kuweza kusahaulika, yeye anaelezea kuwa Hadith, ambayo pia ipo hatarini kupotea, basi ni lazima ziandikwe. Katika uhusiano huu yeye anaelezea aya zifuatazo za Qur’an 2:282, 6:91 na 31:157. 1
Al-Tahawi, pia anaelezea akitoa Aya: "Wala msipuuze kuandika, mapatano yawe ni madogo au makubwa mpaka muda wake.." (2:282) kuhusu uandishi wa madeni, anasema kuwa pale Mwenyezi Mungu anapotuamrisha kuandika madeni ili kuepukana na kutokezea mashaka na mizogo, na uhakika wa elimu ambavyo pia kuuchunga kwake ni vigumu kabisa na muhimu mno kuliko kurikodi madeni basi inasimama pamoja na umuhimu mno katika kuandikwa ili kuepukana na mashaka yaliyoelezwa hapo juu. Abu Hanifa, Abu Yusuf na Muhammad ibn al-Hasan al-Shaybani pia ni watu waliokuwa na msimamo kama huo.2