Aya 23-30: Nuh
Maana
Kila yaliyokuja kwenye Aya hizi yametangulia kutajwa katika Juz. 12 (11: 25-49) yamemaliza zaidi ya kurasa 22, kwa hiyo hapa tutazipitia juu juu tu.
Na hakika tulimtuma Nuh kwa watu wake, akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Hamna mungu asiyekuwa Yeye. Basi je, hamna takua?
Aliwalingania kwenye ibada ya Mwenyezi Mungu peke yake na kuwahadharisha na shirki. Wale wapenda anasa wakahofia vyeo vyao na chumo lao. Wakaanzisha kampeni za uongo na kuwatatiza watu kwa shubha za ubatilifu. Mwenyezi Mungu amezitaja tatu miongoni mwazo:
1. Wakasema wale wakuu waliokufuru: Huyu si chochote ila ni mtu tu kama nyinyi, anataka kujipatia ubora juu yenu.
Walisema, vipi Nuh awe ni nabii naye ni mtu kama nyinyi. Yeye hana lengo la utume katika mwito wake isipokuwa anataka kuwa raisi na nyinyi muwe raia wake. Hii ndio lugha ya wafanyi biashara, wanafasiri faida katika kila kitu.
2. Na lau Mwenyezi Mungu angelipenda, hakika angeliteremsha Malaika. Hatukuyasikia haya kwa mababa zetu wa kwanza.
Hawakusikia kuwa Mwenyezi Mungu alituma mitume, vilevile hawakusikia kuwa Mungu wa ulimwengu wote ni mmoja. Kwa hiyo Nuh si Mtume na miungu ni mingi, yakiwemo masanamu yao. Hakuna tofauti baina ya mantiki haya na mantiki ya anayesema: mimi siamini kuweko kwa sayari ya Mars kwa sababu sijafika huko.
3. Huyo si lolote ila ni mtu mwenye wazimu.
Walileta uongo huu wakijua fika kuwa ni uongo; kama walivyokuwa maquraishi na uhakika wa wa uzushi wao pale waliposema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) amerogwa na ni mwendawazimu.
Basi ngojeni kwa muda. Yaani mngojeni Nuh afe au awache mwito wake.
Akasema: "Mola wangu! Nisaidie kwa kuwa wamenikadhibisha.
Alikimbilia kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu na akamtaka msaada baada ya kukata tamaa na kuongoka kwao.
Tukampa wahyi: Tengeneza jahazi mbele ya macho yetu.
Ni kinaya cha kuichunga kwake Mwenyezi Mungu safina. Na wahyi wetu yaani na amri yetu.
Basi itakapokuja amri yetu na ikafurika tanuri; yaani maji yatakapochimbuka kutoka ardhini.
Hapo waingize wa kila namna dume na jike, wawili na ahli zako, isipokuwa ambaye kauli imekwishatangulia juu yake katika wao.
Yaani isipokuwa mke wake Nuh na mwanawe ambaye inasemekana jina lake ni Kanani.
Wala usinitajie hao waliodhulumu, Hakika wao watagharikishwa.
Yaani usiniombe kuokoka wale ambao neno la adhabu limekwishahakika kwao; hata mkeo na mwanao pia.
Na utakapotulia wewe na walio pamoja nawe jahazini, sema, sifa njema (Alhamdulillah) ni za aliyetuokoa na watu madhalimu.
Katika Aya hii kuna somo muhimu sana, nalo ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anapomwangamiza taghuti haitakikani kunyamaza yule aliyedhulumiwa; bali amuhimidi Mwenyezi Mungu kwa kuokoka kwake na kuangalia kuangamia kwake kuwa ni nyenzo tu sio lengo.
Na sema: Mola wangu! Niteremshe mteremsho wenye baraka na wewe ndiye mbora wa wateremshaji.
Niteremshe kutoka jahazini kwa namna ambayo utanihifadhi na uovu mimi na watu wangu na aliyeamini, kwani wewe ni mtermshaji na muhifadhi bora.
Hakika katika hilo kuna ishara na kwa hakika sisi ni wenye kuwafanyia mtihani.
Yaani sisi tumewafanyia mtihani waja kwa kuwapelekea mitume na kuteremsha vitabu, ili kupambanua muovu na mwema na aonekane wazi wazi kila mmoja wao alipwe thawabu au adhabu, kiasi anachostahiki.
ثُمَّ أَنْشَأْنَا مِنْ بَعْدِهِمْ قَرْنًا آخَرِينَ {31}
فَأَرْسَلْنَا فِيهِمْ رَسُولًا مِنْهُمْ أَنِ اعْبُدُوا اللَّهَ مَا لَكُمْ مِنْ إِلَٰهٍ غَيْرُهُ ۖ أَفَلَا تَتَّقُونَ {32}
وَقَالَ الْمَلَأُ مِنْ قَوْمِهِ الَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِلِقَاءِ الْآخِرَةِ وَأَتْرَفْنَاهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا مَا هَٰذَا إِلَّا بَشَرٌ مِثْلُكُمْ يَأْكُلُ مِمَّا تَأْكُلُونَ مِنْهُ وَيَشْرَبُ مِمَّا تَشْرَبُونَ {33}
وَلَئِنْ أَطَعْتُمْ بَشَرًا مِثْلَكُمْ إِنَّكُمْ إِذًا لَخَاسِرُونَ {34}
أَيَعِدُكُمْ أَنَّكُمْ إِذَا مِتُّمْ وَكُنْتُمْ تُرَابًا وَعِظَامًا أَنَّكُمْ مُخْرَجُونَ {35}
هَيْهَاتَ هَيْهَاتَ لِمَا تُوعَدُونَ {36}
إِنْ هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا نَمُوتُ وَنَحْيَا وَمَا نَحْنُ بِمَبْعُوثِينَ {37}
إِنْ هُوَ إِلَّا رَجُلٌ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّهِ كَذِبًا وَمَا نَحْنُ لَهُ بِمُؤْمِنِينَ {38}
قَالَ رَبِّ انْصُرْنِي بِمَا كَذَّبُونِ {39}
قَالَ عَمَّا قَلِيلٍ لَيُصْبِحُنَّ نَادِمِينَ {40}
فَأَخَذَتْهُمُ الصَّيْحَةُ بِالْحَقِّ فَجَعَلْنَاهُمْ غُثَاءً ۚ فَبُعْدًا لِلْقَوْمِ الظَّالِمِينَ {41}