Welcome

Al-Islam.org needs your financial support to maintain this site & develop new features. Click here to donate generously.

What's New

 • Uchunguzi Juu Ya Uwahhabi

  Kitabu hiki kina eleza juu ya Imani sahihi ya waislamu juu ya maada ya Tauhidi; pia inaeleza  jinsi upotofu katika ufahamu wa Tauhid uliletwa na kikundi cha Wahabi wanao chukua fikra zilizo letwa na Ibnu Taymiyyah (aliye zaliwa mwaka wa 661 A.H.)  ambaye alipingwa katika zama zake na wanachuoni wengi pamoja mababa zake na ufahamu potofu huo uliweza kupotea kabisa. Lakini baada ya miaka 450 fikra hii iliibuliwa na Abdul Wahhab (aliye zaliwa mwaka wa 1115 A.H.)  na zimesaidiwa na wakoloni ili kuleta mfarakano wa fikra ambayo inaendelea mpaka hivi sasa. Kitabu hiki kime-eleza kwa kina Imani Sahihi na Imani Potofu. Msomaji atanufaika sana akii-fuatilia kwa umakini.  

 • Usawa

  Kijitabu hiki kinazungumzia jinsi Imam Ali alivyokuwa anaonyesha usawa kati ya watu wote bila kujali rangi au utajiri wa mtu.

 • Uharamisho Wa Kamari Katika Islam

  Uharamisho Wa Kamari Katika Islam Makala haya yamekusanywa na kutarjumiwa na: Amiraly M.H. Datoo (PO Box 838 Bukoba, Tanzania) Kitabu hiki kinazungumzia uharamisho wa kamari katika Islam kwa kuangalia Quran na hadith. Pia kinaongelea sababu za kamari kuharamishwa katika Islam na athari zake kwenye maisha ya mwanadamu na jamii kwa ujumla. Maneno Mawili Ninamshukuru Allah swt pamoja na Mtume Mtukufu s.a.w.w. na Ahli - Bayt Toharifu a.s. kwa kunijaalia neema hii ya kuweza kukitarjumu kijitabu hiki juu ya maudhui haya ya kamari ili kuweza kuwafaidisha wanaadamu wenzetu ili nao waweze kujiokoa na janga hili kubwa linaloangamiza watu pamoja na famili zao zikiteseka kizazi baada ya kizazi. Mimi binafsi nimewaona wajukuu ambao mpaka leo wanateseka kwa ajili ya madhambi ya mababu zao. Vile vile hapa mjini kwetu nilikuta watu wenye mapesa wakiongoza katika makundi yao ya kucheza kamari kwa mapesa, yaani Waislamu ndio waliokuwa wakiendesha madanguro hayo. Kwa hakika nilijaribu

 • Tawba

  Kitabu hiki kinazungumzia Tawba katika Islam, fadhila zake na faida zake katika maisha ya mwanadamu. Pia kinajadili jinsi ya kutubu tulivyofundishwa na Quran, Mtume Muhammad (SAW) na Aimma.

 • Swali La Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy Na Jibu La Imam Muhammad Husain Kashiful Ghitaa wa Najaf

  Makala hii inajibu swali la mwanachuoni maarufu wa Afrika Mashariki kuhusu hadhi ya masahaba wa Mtume (s.a.w.w.). Swali limejibiwa na mwenye umahiri wa kielimu na uchamungu wa hali ya juu, aliyeishi katika nchi ya Iraq na aliyehudumia Uislamu na Waislamu kwa zaidi ya miaka 40.

 • Tadwin Al Hadith

  Hadithi ni chanzo cha pili muhimu cha Sheria na Hukmu katika uislam. Makala hii inaelezea jinsi chanzo hiki muhimu kilivyovurugwa na ni jinsi gani wapokezi wa hadithi walikatazwa kuandika hadithi za Mtume s.a.w.w. La kushangaza ni kwamba wale walioonekana kuwa karibu na Mtume s.a.w.w zama za uhai wake wakawa ndio waliotoa amri ya kuzuia hadithi zisiandikwe na kutumiwa kama rejea baada ya kifo cha bwana Mtume s.a.w.w. Madhara ya jambo hili yanaonekana wazi katika zama hizi tulizonazo. Ni imani kuwa uelewa wa wasomaji utapanuka baada ya kusoma makala hii.

 • Shada La Maua Kutoka Bustani Ya Ahadith Za Mtume & Ahlul – Bayt

 • Sifa Za Wamchao Allah (swt)

  Sifa Za Wamchao Allah (swt) Makala haya yamekusanywa na kutarjumiwa na: Amiraly M.H. Datoo (PO Box 838 Bukoba, Tanzania) ***** Makala hii ni sehemu moja ndogo kutoka kitabu kitakatifu cha Nahjul-Balagha, ambacho ni kitukufu baada ya Qur’an Tukufu, chenye maandiko ya Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Makala inatueleza sifa za Wachamungu na ni mwongozo kwa sote. ***** Hotuba ya Imam Ali ibn Abu Talib a.s. kutoka Nahjul Balagha Ifuatayo ni Hotuba Na. 193 ya Imam Ali ibn Abu Talib a.s. kutoka Nahjul Balagha (Sharh ya al- Hadid, Vol. 10, uk. 132-162). Imeripotiwa na Sahaba wake Amir al-Mu'uminiin Ali ibn Abi Talib a.s. aliyekuwa akiitwa Hammam ibn Shurayh ambaye alikuwa mcha Mungu sana. Alimwambia Imam Ali a.s. "Ewe Amir al-Mu'uminiin, nielezee sifa za Muttaqiin (Wacha Mungu) kwa hali ambayo kama kwamba ninawaona wao." Imam Ali a.s. alijaribu kusita katika kumjibu na alimwambia, "Ewe Hammam, mwogope Allah swt na utende matendo mema kwa sababu Allah swt anasema katika

 • Wito Kwa Waislamu Kuuendea Ukweli

  Makala haya yanaeleza kwa kina kuwa mrithi wa haki wa Mtume (s.a.w.w.) baada yake ni nani na dalili zote zime tolewa kutoka vitabu vya Sahihi na vinavyo tegemewa na kurejewa.

 • Semi Za Imam Ali [a.s.]

  Semi Za Imam Ali [a.s.] ***** Kitabu hiki kilichokuwa mikononi yako ni mkusanyiko ya semi za Amirul Muuminin Ali Bin Abu Talib a.s. Semi hizi ni mwongozo bora mno kwetu na ime elezwa katika kitabu Ma’anil Akhbaar na Imam Ali ar-Ridha a.s. kuwa, “Kwa hakika, iwapo watu wangelikuwa wamezijua faida na mema ya semi zetu, basi kwa hakika wangelitufuata sisi.” Atakayesoma kitabu hiki ataelewa faida na thamani yake kubwa ya kidini na akizingatia, maisha yake yatakuwa mema sana. ***** Dibaji Mtukufu Amirul Muuminin (Bwana wa Waumini) alizaliwa miaka 23 kabla ya Hijriya (sawa na mwaka 599 Miladia) mjini Makka. Mnamo tarehe 21 Ramadhan mwaka 40 Hijria (mwafaka Januari 24, 661 Miladia), wakati wa sala ya asubuhi, aliuawa shahidi na Abdul Rahman ibn Muljim Muradi katika mji wa Kufa na akazikwa katika mji wa Najaf ulio karibu na Kufa (Iraq). Imam Ali (a.s.) ni mkwe wa Mtume Muhammad (s.a.w.) na ni mmojawapo kati ya watu wenye hekima kubwa kabisa katika Uislamu. Si kwamba

Mpya/ngeni katika Uislamu?

Kugundua Uislamu kwa kuvinjari kwa kuchaguwa vyanzo (material) kutoka maktaba yetu iliyo sahihi hasa kwa wale ambao kwao Uislamu ni mpya/geni . Kutambulisha Uislamu | Desturi za Waislamu | Maisha ya Kiroho | Uislamu na Ukristo | Kubadilika na kuwa Mwislamu

Ni nani Shi'a na Sunni?

Kuelewa ufanano/uweo na tofauti kati ya fikira kuu mbili [ya mawazo] katika Uislamu, na kujua zaidi kuhusu Uislamu kama ilivyo fundishwa na Mtume na familia yake. Kuwa tambulisha Ahlul bayt (Familia ya Mtume (S) | Umoja kati ya Shi’a na Sunni | Imani ya Shi’a Kuelezwa | Mijadala & Majadiliano | Majibu ya Imani Potofu | Kwa nini wakawa Shi'a | Vyanzo kwa ajili ya Utafiti Zaidi

Muharram na Karbala

Vyanzo vinavyohusiana na Mwezi wa Muharram, na Janga ya Karbala History of Ashura | Imam Husayn and his Martydom | The Excellences of the Imam Husayn in Sunni Hadith Tradition | Mukhtar al-Thaqafi | The Revolution of Imam al-Husayn (a)

Timeline

Sign up for Al-Islam.org newsletter

Sign up to get notified when new books & articles are added to Al-Islam.org

Our Sub Projects