Kitabu kilichoko mkononi mwako ni tarjumi kutoka lugha ya Kiarabu ya kitabu maarufu katika ulimwengu wa Kiislamu, Nahju 'l-Balaghah. Kitabu hiki kitachapishwa katika majalada mbali mbali, na hili ulilo nalo mkononi ni jalada la kwanza.

Nahju 'l-Balaghah ni mkusanyiko wa khutba, barua na maelekezo ya Imam Ali (a.s.). Mengi yamesemwa kuhusu ubora na ufasaha wa maneno yaliyomo katika khutba na harua hizo. Kwa ufupi, Nahju 'l-Balaghah ni kilele cha ufasaha.