Kitabu hiki kina eleza juu ya Imani sahihi ya waislamu juu ya maada ya Tauhidi; pia inaeleza  jinsi upotofu katika ufahamu wa Tauhid uliletwa na kikundi cha Wahabi wanao chukua fikra zilizo letwa na Ibnu Taymiyyah (aliye zaliwa mwaka wa 661 A.H.)  ambaye alipingwa katika zama zake na wanachuoni wengi pamoja mababa zake na ufahamu potofu huo uliweza kupotea kabisa.
Lakini baada ya miaka 450 fikra hii iliibuliwa na Abdul Wahhab (aliye zaliwa mwaka wa 1115 A.H.)  na zimesaidiwa na wakoloni ili kuleta mfarakano wa fikra ambayo inaendelea mpaka hivi sasa.
Kitabu hiki kime-eleza kwa kina Imani Sahihi na Imani Potofu. Msomaji atanufaika sana akii-fuatilia kwa umakini.