Hadithi ni chanzo cha pili muhimu cha Sheria na Hukmu katika uislam. Makala hii inaelezea jinsi chanzo hiki muhimu kilivyovurugwa na ni jinsi gani wapokezi wa hadithi walikatazwa kuandika hadithi za Mtume s.a.w.w. La kushangaza ni kwamba wale walioonekana kuwa karibu na Mtume s.a.w.w zama za uhai wake wakawa ndio waliotoa amri ya kuzuia hadithi zisiandikwe na kutumiwa kama rejea baada ya kifo cha bwana Mtume s.a.w.w. Madhara ya jambo hili yanaonekana wazi katika zama hizi tulizonazo. Ni imani kuwa uelewa wa wasomaji utapanuka baada ya kusoma makala hii.