read

Hii ni makala juu ya vijana na bangi. Makala hii pia anatuambia kwanini vijana wanatumia bangi.

Bangi Yaua Na Yaimarisha Ukoloni

"Moja... Mbili... Tatu...
"Aa! Nzuri kabisa! Tumekuwa malaika, hamhisi hivyo?"
"Ndiooo!! Ndiooo!!"
"Basi njooni turuke mbinguni."
"Hiyo ni fikra nzuri. Haya na turuke!
"Moja... Mbili. .. Tatu..."

Vijana watano wanachupa kutoka ghorofa ya kumi na tisa, wanakatika vipandevipande na nyama na mifupa kutawanyika.

Mama watano wanaingiwa na majonzi ya vijana wao ambao baada ya kuvuta bangi wali­pandwa na nishai na walijiona kuwa ni malaika na kwamba wangeweza kuruka.

Wasichana na wavulana huvua nguo zao hadharani na kufanya vitendo vichafu, kisha hucheza wakiwa uchi huku watoto wakiwa­zunguka na wakiwatupia maganda ya ndizi na kuwacheka!

Kijana asiyezidi umri wa miaka kumi na tano hukaa kwenye baraza la nyumba yao iliyoelekea mashariki, akilikodolea macho jua kwa muda wa masaa mengi huku akiimba: "Mwezi weee!! Mwezi weee!!. . ." mpaka huchoka kiasi ambacho huwa yu hoi kabisa. Hupelekwa hospitali na kuonekana kuwa amepofuka macho kiasi ambacho hawezi kutibiwa.

Katika siku moja asubuhi, mtu mmoja mwenye umri wa miaka hamsini alitangaza kwamba alikuwa nabii wa mwisho, na kwamba utume wake unahusu wajibu wa "ibada ya mwanamke!"

Usiku wa manane wa siku hiyohiyo, watu wakasikia sauti ya ugomvi ikifuatiwa na sauti ya kuugua. Asubuhi ilipopambazuka, ikabainika kwamba mtu huyo amemwua mke wake usiku ule.

Hivyo ndivyo bangi, kasumba na vileo vingine vinavyowafanya watu!

Na hiyo ndiyo hali waliyoizoea watu katika nchi ambazo vileo hutumiwa kwa wingi sana, kama vile Marekani, Sweden na Thailand.

Afyuni, heroini au bangi, kwa mfano, humpumbaza mtu na ikampa nishai akawa anawaza mawazo mbalimbali mpaka kujifikiria kuwa yeye ni malaika, nabii au kwamba ana ahadi kuutongoza mwezi kumbe ni jua!

Kisha heroini humfanya mtu afanye vile mawazo yake yanavyompumbaza na kumwam­risha; hujaribu kuruka kutoka kwenye paa ya nyumba kuelekea mbinguni, na matokeo yake huanguka chini na kuvunjikavunjika mifupa yake na kufa. Au humfanya aliimbie jua nyimbo za mapenzi huku akilitazama kwa muda mrefu mpaka akapofuka macho. Au anawalingania watu wamwabudu mwanamke wakati wa asu­buhi, kisha humwua mkewe usiku wa manane.

Namna hii ndivyo heroini inavyoondoa utu wa mtu.

Lakini je, ni heroini tu ndiyo inayoondoa utu? Je, pombe nayo inamwathiri vipi mlevi?

Tukiachilia mbali madhara yanayoletwa na pombe kwa maini na mishipa ya fahamu (neva) na jinsi athari yake ilivyo mbaya, utaona kwamba daktari humwuliza mgonjwa wa ini, macho au neva: "Je, unakunywa pombe?" Akikataa humwuliza: "Je, baba yako vipi?" Akikataa humwuliza: "Je, babu yako alikuwa akilewa?" Akisema ndiyo, husema: "Huo ni ugonjwa wa kurithi!"

Tuyawache yote hayo na tuzungumzie mato­keo yanayoletwa na ulewaji katika jamii.

Hapana shaka kwamba pombe ina ladha nzuri kwa mnywaji. Na tukichukulia kwamba pombe haidhuru siha ya mtu na akili yake na kwamba athari yake ni ya muda tu, basi hapo tujiulize, je, athari ya jamii ikoje?

Je, jamii inalazimika kuvumilia athari za hatari kwa sababu mtu fulani anapata "utamu wa ulevi?"

Kazi ya wizi pia ina Iadha kwa mwizi, lakini athari yake ya kijamii ambayo huharibu mizani ya uadilifu ndiyo inayotufanya tumwadhibu mwizi.

Vivyo hivyo kwa pombe.

Pombe ni tamu kwa mlevi, humpeleka mnywaji kwenye ulimwengu mzuri wa mawazo! Lakini kwa wakati huohuo inaidhuru jamii kwa kuwafanya baadhi yao wakose kutekeleza
wajibu wao kwa wakati maalum.

Mara ngapi tunasikia mashtaka katika mahakama hakimu akimwuliza mshtaki:

"Je, amemwua mwanao kwa gari lake?"

"Ndiyo."

Lakini mshtakiwa huyo hazingatiwi kuwa ni mwuaji, kwa sababu wakati huo alikuwa katika hali ya ulevi, hivyo hahesabiki kuwa ni mwuaji kwa vile hakuweza kujizuia na kitendo hicho.

Kwa hivyo, ulevi umekuwa ni udhuru wa kisheria kumwepusha mhalifu na kosa lake. Bali wahalifu wengine baada ya kufanya uhalifu wao hunywa pombe ili waepukane na hukumu, au hunywa pombe kisha akatenda uhalifu wake.

Sasa hebu tujiulize: Kwa nini tuwaache baadhi ya watu wafanye vile wanavyotaka kuwa­dhuru watu lakini wanapotiwa mkononi wasi­hesabiwe kuwa wamekosa?

Hivi karibuni katika nchi moja jirani kime­pita kisa hiki cha kusikitisha:

Saa tisa ya usiku mmoja, wakati kijana mmoja mwenye umri wa miaka kumi na nane alipokuwa akitalii masomo yake kwa ajili ya mtihani huku akiwa ameshughulika kufungua kurasa za kitabu chake kwa matumaini ya kufa­ulu mtihani wake na kufikiria mustakabali wa maisha yake, mara gari lililokuwa likiendeshwa na vijana watatu walevi liliacha njia na kuelekea upande wake, likamgonga kwa nguvu na kumtupa upande mwingine na kuchanachana kitabu chake. Kisha gari likageuka tena na kugonga gari la mhandisi mmoja na kuliharibu.

Mmoja wa vijana watatu hao alipatwa na jeraha ndogo kichwani. Vijana wakasimamisha gari lao na wakatoka nje kwa pamoja si kwa ajili ya kumsaidia kijana aliyejeruhiwa au kutengeneza hari lao, bali kwa ajili ya kuimba na kucheza mchezo wa Bob Hope. Hayo ni matokeo ya ulevi.

Siku iliyofuatia, kijana mwanafunzi alione­kana akitolewa kutoka chumba cha operesheni akiwa amekatwa mguu wake wa kuume kutokana na jeraha la hatari alilolipata kwa ajali hiyo; na wakati huohuo, vijana watatu walitoka kwenye ukumbi wa mahakama baada ya kuhukumiwa kulipa faini ndogo tu kwa vile walikuwa wame­lewa!

Tatizo haliishii hapo tu! Kwani walevi wa chang'aa hawatosheki na pombe tu, bali hutafuta kileo kingine chenye kulevyesha zaidi, hivyo huanza uraibu wa kuvuta bangi.

Mwendo wa "ukarimu" wa wavuta bangi kukaribishana bangi umeufanya uvutaji wa bangi uenee haraka sana katika dunia, mpaka watoto pia wakaanza kuvuta bangi!

Kwa vile matokeo ya uvutaji bangi yamekuwa ya kutisha sana, wataalamu wa elimujamii, madaktari na wanafikra wakafanya semina kadhaa kulijadili suala la saratani hii mpya ambayo inaenea na kuua, na kumfanya mvutaji ahisi utamu wa kufa kwake!

Vifaa vya kipolisi na vikosi maalum vika­undwa kupambana na utumiaji na vileo na viwanda vikaanza kutengeneza vifaa vya kugu­ndua madawa ya kulevya katika mizigo ya wasa­firi. Mbwa bora wa polisi wakafunzwa kunusa heroini. Habari za kukamatwa kasumba, heroini, bangi, n.k. zimekuwa zikiandikwa kila siku katika magazeti ya kila mahali na kupewa uku­rasa maalum katika magazeti mengi ulimwenguni. Polisi wamekuwa wakibadilishana mawazo juu ya njia za kukabiliana na uraibu huo. Nchi kadhaa zikajenga hospitali mahsusi kwa ajili ya kuwatibu waraibu wa vileo. Somo maalum kuhusu uraibu wa vileo likaanzishwa katika kitivo cha utibabu kuchunguza hali za waraibu wa kasumba, bangi, n.k.

Lakini pamoja na yote hayo, wavutaji na watumiaji kasumba wamekuwa wakiongezeka, na kila siku idadi yao inazidi.

Kwa mujibu wa takwimu ya karibuni, idadi ya waraibu wa bangi na vileo vinginevyo imefikia watu milioni 400!

Kwa nini juhudi zote hizo hazikufanikiwa?

Kwa sababu walikuwa wakichungua matokeo na madhara yake tu, bila ya kuchungua sababu zake. Walikuwa wakipambana dhidi ya "matunda mabaya" wakati ambapo wanatakiwa kutibu mizizi mibaya.

Hebu sasa tuchungue chanzo na sababu zinazowafanya vijana kuvuta bangi na kasumba na kulewa.

Nafikiri sababu za msingi zinazowafanya vijana wavute bangi ni hizi zifuatazo:

Kwanza: Faragha.
Pili: Uhitaji.
Tatu: Uigaji.
Nne: Ukoloni.

1. Faragha

Zamani mtu alikuwa akifanya kazi wakati wote kwa ajili ya kupata tonge la kuishi. Muuza duka alikuwa akifanya biashara asubuhi na jioni - na pengine hata usiku - ili kupata riziki ya kuweza kumtosha na anaporudi nyumbani huwa amechoka kabisa na hafikirii kitu chochote isipokuwa usingizi tu!

Hivyo ndivyo yalivyokuwa maisha ya wafa­nyakazi, wafanyabiashara na hata wanafunzi.

Lakini leo baada ya viwanda kuchukua mahali pa mikono ya watu, na kiwanda kimoja tu kuweza kutekeleza chenyewe kazi za watu elfu moja, masaa ya kazi yamepungua pia.

Kwa kawaida mtu anafanya kazi masaa manane.

Tukisema kwa mfano, mtu hulala kwa masaa manane na hula kwa masaa mawili, yatabaki masaa sita - yaani masaa 180 kila mwezi.

Sasa masaa hayo anayatumia wapi?

Pengine watu waliooa wanaweza kuyatumia vizuri masaa hayo pamoja na wake zao na watoto wao, lakini je, makapera na wanawali ambao wengi wao ni vijana, wanayatumia wapi masaa hayo?

Kwa hivyo, "suala la faragha" - yaani kuwa na wakati - ni miongoni mwa masuala ya hatari sana ambayo yanajadiliwa na wataalamu wa elimujamii, elimunafsi na elimujinai (criminol­ogy), kwa sababu kimaumbile mtu yuko dhidi ya faragha na hawezi kukaa bure bila ya kufanya kitu.

Ikiwa mtu atakuwa na muda wa faragha, basi muda huo unaweza kumdhuru kama vile tumbo la chakula linapokaa bure bila ya kufanya kazi ya kuyeyusha chakula huanza kujiyeyusha lenyewe!

Kwa hivyo, binadamu huathirika kimaada, kiroho, kinafsi na kimatendo kama tumbo.

Ni kweli kwamba haiwezekani wakati wote mtu kuwa katika hali ya harakati na juhudi, ijapokuwa maisha yote ni ya juhudi, lakini pia haitakikani kwa mtu kujidhoofisha, kwani hapana budi kupatikana kitu kitakachoziba wasaa wake.

Kumfunga mtu mmoja peke yake katika seli moja ya jela kunachukuliwa kuwa ni adhabu kubwa sana - kwa nini?

Kwa sababu kila wakati wa mtu ukipita bure bila ya kufanya kitu cha faida, wakati huo humwangamiza.

Ndiyo maana Uislamu umesema haya kwa kauli ya Mtume Mtukufu SAW:

"Hakika mimi sipendi yeyote kati yenu ahangaike isipokuwa katika mambo matatu:

1) Kuwa na lengo katika maisha; 2) Kupiga hatua kwa ajili ya Akhera; au 3) Kustarehe katika mambo yasiyokuwa haramu."

Maana ya hadithi hii ni kwamba mtu ayapitishe juhudi zake katika mikondo mitatu: "Mkondo wa maisha," "mkondo wa amali njema" na "mkondo wa starehe zilizo halali."

Swali: Je, ni starehe zipi hizo zilizohala­lishwa?

Jawabu: Ni kila starehe inayomnufaisha mtu na jamii yake bila ya kuwaletea dhara lolote, kama vile: Starehe zako pamoja na mkeo au pamoja na watoto wako. Starehe zako katika kusoma, kutunga vitabu, kusafiri, kucheza michezo yenye faida, kama vile riadha na mazoezi ya mwili, kuogelea, kupanda farasi, n.k. Starehe katika kukusanya stempu na picha, na kukutana na marafiki na kutembeleana.

Zote hizi ni starehe zilizohalalishwa katika Uislamu. Mtu anatakiwa kutumia wakati wake wa faragha katika starehe kama hizo badala ya kukaa bure, kwani haiwezekani daima awe katika juhudi bila ya kujistarehesha kiwiliwili na kifikra.

Ikiwa mtu atakaa bila ya kufanya kitu chochote katika wakati asiokuwa na kazi, basi itabidi autumie wakati huo kwa kuvuta bangi, au kunywa pombe au kufanya kitu chochote kisichokuwa na faida.

Je, umemwona mtoto anafanya nini anapokosa la kufanya au anapokosa kucheza na wenzake?

Hupiga kelele, hurukaruka ovyo, huvunja vyombo, au huharibu ukuta.

Basi vivyo hivyo kwa watu wazima. Je, watu wazima si watoto wakubwa?

Imethibitishwa kisayansi kwamba nafsi ya faragha (kukaa bure) yaua. Na inaaminiwa kwamba idadi ya watu wanaokufa ambao
hawafanyi kazi ni zaidi kuliko ya wale wanaoji­shughulisha mpaka uzeeni.

Kwa hivyo, huwezi kumpata mtu mwenye umri mrefu isipokuwa awe ni yule mwenye kufanya kazi kila siku kama mkulima, mjenzi, n.k.

2. Uhitaji

Mtu anapokosa mahitaji ya lazima ambayo ni dharura kwa ajili ya maisha yake, huwa ana­ona dhiki na uzito wa maisha, na huhisi unyonge, uhitaji na maonevu.

Kama watu wote wangekuwa wanakosa mahitaji ya lazima, basi mtu asingehisi uhitaji, na hisia za kuhitaji zingekuwa katika mwelekeo sahihi wa kufanya kazi kwa pamoja ili kuondoa shida yake na kukidhi mahitaji yake.

Maadamu watu wote ni wahitaji, basi kila mmoja wao pia ni mhitaji.

Na maadamu watu wote wanafanya kazi kuondoa shida zao, basi kila mmoja wao atafanya kazi pamoja nao.

Hapa ndipo tunapoona kwamba watu wanapohisi uhitaji, huanza kutafuta njia za kuondoa hisia hiyo.

Mtu hujihisi mnyonge akiona hapati mahitaji ya lazima wakati ambapo anawaona wengine wanapata wanayoyahitaji na yale wasiyoyahitaji pia. Hapo roho ya mtu husumbuka - ama huijenga au huibomoa.

Huijenga nafsi na jamii yake kwa kuhangaika ili kukidhi mahitaji yake.

Au huiharibu nafsi na jamii yake kwa kuele­kea kwenye bangi, kasumba, pombe na vitu duni.

Unaweza kumwona mtu anamiliki majumba kadhaa, lakini pamoja na hayo bado anajenga majumba marefu kana kwamba anataka kuzi­meza ardhi na mbingu, wakati ambapo mtu mwingine hapati hata chumba kimoja cha kulala kwa raha kwa sababu ya kukerewa na mwenye mali. Hapana shaka mtu huyo atahisi uonevu tu!

Hisia ya uhitaji na unyonge hutokeza katika watu ambao huona mamilioni ya shilingi yamelala katika mabenki na wanayatumia mamilioni mengine katika starehe wakati wanahitajia shilingi kidogo tu!

Kuna maskini wasiomiliki kitu ila dhiki na shida.

Na kuna mabepari waliokaa kimya.

Katika hali ya uhitaji na unyonge mtu huona dhiki.

Kama kungekuweko mwamko mzuri, basi hapana shaka hisia hiyo ingekuwa ni chanzo cha
kufanyika kazi nzuri kama ilivyokuwa nchini Japan. Watu wa Japan walikuwa katika “dhiki" kwa sababu walikuwa wakihitajia “malighafi” na “viwanda vidogovidogo". Nchi yao ilikuwa maskini kiasi ambacho haikuwoza kujitosheleza, ikawa inaagizia mahitaji yake yote kutoka nje na tena kwa gharama kubwa.

Akatokea mfalme mmoja ambaye alikuwa akiheshimiwa sana na watu, na akazuwia uingizaji wa vitu kutoka nje ili kujiepusha na gharama. Mfalme aliulizwa na wananchi:

“Ewe mfalme mtukufu! Vipi tutazuia vitu vya nje wakati ambapo tunaagizia hata viatu na hata viatu vya mfalme pia vinatoka nje?”

Mfalme akahisi huo ni uhitaji na unyonge, hivyo akavitupa viatu vyake na akasema:

“Kwa vile hatutengenezi viatu, basi hakuna haja ya kuvaa viatu.”

Naye akawa mfalme wa keanza kutembea bila ya viatu!

Na hatua hiyo ikawa ndiyo chanzo cha maendeleo ya viwanda katika Japan.

Hayo yanatokea kama kuna mwamko.

Na kama hakuna mwamko wowote mzuri, basi hisia za unyonge na uhitaji zitambomoa yule mwenye kuwa nazo.

Vijana wanaelekea kwenye bangi, heroini au vileo vinginevyo ili kukimbia hali ya dhiki na kuelekea kwenye ulimwengu mzuri na mtulivu wa kidhahania (kimawazo) tu.

Kwa vile matatizo ya kweli hayatatuki katika ulimwengu wa mawazo, hivyo kijana mvutaji huwa anajizidishia matatizo yake, kwani pesa anazitumia katika bangi, afyuni na ulevi humzidishia matatizo yake na uhitaji.

Kwa hivyo, huendelea kutumia vileo mpaka kuwa mraibu.

Mwisho wake huwa mvivu akizurura usiku na mchana kutafuta starehe na matamanio yasiyokwisha mpaka akamalizikiwa na nguvu zake zote.

3. Ugaji

Nilimwuliza kijana mmoja mvuta bangi:

"Umeanza lini kuvuta bangi?”

“Sikumbuki, lakini nakumbuka sigara ya kwanza nilipata bure kutoka kwa rafiki yangu; na nilianza kuvuta bangi pamoja na kikundi cha wenzangu.”

“Na hivi sasa je?”

“Ni mvuta bangi namba wani.”

“Unatumia kiasi gani kwa ajili ya bangi?”

“Theluthi moja hadi nusu ya mshahara wangu.”

"Mshahara wako ni kiasi gani?"

"Dinari 120."

"Yaani inafika ukatumia Dinari 60 kwa mwezi?"

"Ndiyo, bunda moja siku hizi ni ghali sana."

“Bei gani bunda moja?"

"Inategemea upatikanaji wa bangi, lakini siyo chini ya Dinari 10, mara nyingine inazidi Dinari 15."

"Vipi na wakati gani unavuta bangi?"

"Wakati gani si muhimu. Wakati wowote ninaweza kuvuta bangi, na hasa usiku. Ama vipi ninavuta, mara nyingi tunavuta tukiwa kikundi, kuiga ni sababu ya watu wengi kuvuta. Kila mmoja humfuata na humwiga mwenziwe."

"Unajisikiaje unapovuta bangi?"

"Naona raha na furaha, na mara nyingine huzuni. Ninaweza kucheka sana na ninaweza kulia sana pia. Inategemea vile bangi itakavyo­mpa mtu nishai, hali zote si sawa. Lakini mimi huwa ninataka utulivu, hivyo tunavuta usiku na tunakaa mahali pasipokuwa na ghasia."

"Zaidi ya hivyo unahisi nini?"

"Ninaweza kuhisi kuwa ninaendesha gari inayotembea barabarani, lakini kumbe nimekaa mahali pengine!"

"Je, mnapata wafuasi wapya?"

"Ndiyo."

"Kwa njia gani?"

"Kwa kufanya urafiki."

"Je, huna nia ya kuacha kuvuta bangi?"

"Hapana."

"Lakini sayansi inasema kwamba kuende­lea kutumia vileo kunapunguza umri wa mtu."

"Hakunishughulishi kupungua umri, kwani ninaona ni bora kuishi miaka 30 ya bangi kuliko kuishi miaka 60 bila ya bangi!"

"Tuchukulie kuwa bei ya bangi imepanda, je utafanya nini?"

"Mimi ninavyojiona niko tayari kumwuza baba yangu na mama yangu ili nipate bangi!"

"Mnapata wapi bangi?"

"Ziko njia nyingi, na walanguzi wa bangi wanaweza kukupatia mahitaji yote ya bangi. Mara nyingine tunalazimika kumtuma mtu nje atuletee."

"Je, kazi hiyo ina usalama?"

"Hapana! Ni hatari sana, lakini kwetu ni sawa tu! Ingawaje wauzaji wengine wa bangi wana maingiliano na serikali, jambo ambalo lina­sababisha kupanda kwa bei ya bangi!"

Kwa hivyo, kulingana na utafiti uliofanywa, sababu kubwa inayomfanya mtu kuvuta bangi ni kumwiga rafiki yake. Kijana akimwona rafiki yake anavuta, na yeye anavuta pia, hafikirii
kuwa kitendo hicho kichafu kitampeleka wapi.

Hata Watoto

Kama vile ambavyo watoto wanakuwa wavutaji sigara kwa kuwaiga marafiki zao, vivyo hivyo wanazoea kuvuta bangi kwa njia hiyo wanapo kua.

Idadi ya watoto wanaovuta bangi inazidi kupanda; watoto hivi sasa wanaanza kuvuta bangi wakiwa bado wadogo sana, kwa hiyo wana­nyauka kama yanavyonyauka majani yaliyo­patwa na upepo wa sumu.

Ikiwa kitabia mtoto huiga, je, mtu mzima atakuwaje?

Kwa nini mtu anakosa uhuru katika kuji­amulia mambo yake kwa kuwaiga watu wengine?

Kwa nini tukose nguvu za kufikiri na kuji­tegemea?

Kisha kwa nini tuwaige wageni katika mambo mabaya na wala tusiwaige katika mambo mazuri?

Watu wanakuwa kama yule mtu mjinga aliye­ingia kwenye kundi la watu wenye afya nzuri akawaona wanakula matofaa, badala ya kula matofaa, alikwenda kula mavi yao.

Hakika ulevi, bangi, afyuni, kasumba na kuvunja ujamaa ni katika maradhi ya utamaduni wa kimaada, basi kwa nini tuyaige?

4. Ukoloni

LSD (lysergic acid diethylamide) ni aina ya dawa mpya ya kulevya. Kiasi cha mfuko mmoja tu wa mkononi uliojaa kileo hiki kinatosha kuwafanya watu milioni mia mbili wa Marekani wawe katika hali ya ulevi kwa muda wa masaa 24.

Basi kwa nini mtu anazoea kutumia kileo hiki?

Wanasema ni kwa ajili ya kupata utamu wa kiroho!

Kwani mtu hawezi kupata angalau kileo kingine chenye madhara machache kuliko kutu­mia kileo hiki kinachopoteza akili ya mtu baada ya wiki chache tu?

Mtu haanzii na LSD moja kwa moja, bali huanza kunywa pombe, kisha anapata uraibu wake, tena anaelekea kwenye bangi.

Anapozoea kuvuta bangi na kuona utamu wake huelekea kwenye afyuni (heroini).

Baada ya kuwa na uraibu wa heroini ndipo huelekea kwenye LSD ambayo mwisho wake ni mauti au wazimu. Haiwezekani kutumia kitu kingine baa da ya LSD, kwani mtu huwa mwenda­wazimu au kiwiliwili kinakosa uzima.

Kwa hivyo, mwanzo wake ni pombe, kisha bangi, kasumba, n.k., na mwisho ni kifo au uwendawazimu!

Je, pombe nayo inamfanya nini mtu? Elimu ya kisasa imetoa orodha ndefu ya madhara yanayoletwa na unywaji wa pombe.

Kwa mfano:

Pombe humfanya mtu aishi katika ulim­wengu wa mawazo mapuuzi tu!

Hayo mawazo mapuuzi yanayosababishwa na ulevi humfanya mtu afadhaike upesi mara tu anapopatwa na jambo asilolipenda. Hivyo humfanya awe na chuki na uchungu.

Ulevi unaathiri ubongo kwa njia iliyo wazi kabisa na unasimamisha kazi yake. Kwa hivyo, ngao ya uhai unaharibika kabisa kwa sababu ya kutumia vileo, na hudhoofisha akili na uwezo wa mtu.

Imethibiti kwamba chanzo cha upotevu wa watu wengi ni athari ya pombe, kwa sababu inapoteza akili na hiari ya mtu na huondoa fahamu na mwamko wake.

Imam Ridha (AS) amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu ameharamisha ulevi kwa sababu ya
uharibifu wake na kupoteza akili katika mambo ya hakika, na kuondoa haya katika uso.”

Kuanzia hapa, ulevi unazingatiwa ni moja­wapo kati ya sababu kubwa za jinai.

lmethibitishwa kwamba 75% ya jinai ya mauaji, 38% ya jinai ya kupiga na kujeruhi, na 82% ya jinai ya kutia moto makusudi yana­sababishwa na ulevi. (al-'Uluumul-Jinaaiyyah, uk. 837).

Pombe inazingatiwa kuwa ni sababu ya kimsingi ya uwendawazimu. Kwa hivyo, idadi ya wendawazimu katika nchi yoyote inaongezeka kulingana na kuongezeka ulevi na mabaa.

Sensa ya mwaka 1934 katika Ufaransa ime­thibitisha kwamba watu laki mbili walipatwa na wendawazimu kwa sababu ya kulewa.

Pombe hurithisha udhaifu wa newa. Dk. Karl amesema: "Ni uhalifu hasa mume na mke kujamiiana katika hali ya ulevi, kwa sababu ulevi unarithisha udhaifu mkubwa wa mishipa ya fahamu katika watoto watakaozaliwa."

Vilevile imethibishwa kisayansi kwamba nusu ya watoto wanaorithi athari za vileo kutoka kwa wazazi wao, hufa upesi kwa sababu ya udhaifu wa kuzuia maradhi.

Sote tunajua vipi Ufaransa ilivyoshindwa katika Vita vya Pili vya Dunia kwa sababu askari wake walizama katika ulevi na ufisadi.

Ufaransa inatengeneza nusu ya vinywaji vya alkoholi (vileo) katika Ulaya, na Ulaya inatenge­neza nusu ya vileo vya dunia nzima. Pamoja na hayo, Ufaransa haitosheki na kiwango cha uzali­shaji huo wa vileo, bali inataka zaidi.

Kwa sababu hii Ufaransa ilianguka na ngome ya Maginot iliyojulikana kwa masaa machache tu ikatekwa!

Tukichukulia kuwa kila shirika linalotenge­neza na kuuza pombe ni shirika la kigeni, tuta­jua kwamba ni pesa ngapi zinakwenda katika mifuko ya mashirika hayo kwa lengo la kuji­rubisha kwa Shetani.

Na ni masaa mangapi katika maisha ya umma yanapotezwa na vijana katika ulevi na sakarani?

Kwa hivyo, hapana budi kuzingatia mambo mawili ya hakika:

Kwanza: Mashirika ya kutengeneza ulevi aghlabu yao ni ya Mayahudi, kama yale mashirika ya kutengeneza filamu za jinsia (seksi) ambayo ni ya Mayahudi pia. Kwa sababu Mayahudi wanaona ni muhimu kwamba watu wengine wawe wanaelekeza mawazo yao kwenye ulevi na vileo ili iwe rahisi kwao kuwatawala. Protokali ya wanavyuoni wa Kizayuni inaeleza waziwazi jambo hili: "Na sisi tunaweka sera ya maadili mabaya mpaka tuwageuze watu wawe ni watu waliopotezwa na pombe, na kuugeuza ujana wao kuwa umeingia wazimu kijinsia na kifisadi. Wawakilishi, walimu na watumishi wetu, na vitabu na wanawake wetu katika majumba ya starehe wataandalia kutimizwa sera hiyo." (Protokali ya Wanavyuoni wa Kizayuni, na. 1).

Pili: Ulevi, wanawake malaya na vileo katika nchi zetu ni mirathi ya kikoloni; na jambo hili halina shaka kwa mtu yeyote.

Sijui kwa nini tufikirie kwamba wakoloni ni watu wenye nia safi kwetu wakati wao wametu­letea vitu hivi na wanajaribu tuvizowee?

Hakika nguvu za kikoloni ziko katika msingi wa kuwajibika kwake kuwatia watu kasumba na pia kuwafanya wazowee vileo.

Kwa hivyo, si vigumu kwa wakoloni kuwa­tawala watu kupitia njia hizo.

Ndiyo maana ukoloni umeleta katika nchi zetu vileo na mila ya kutembea uchi na mambo mengine machafu ambayo yanawafanya watu wakose nguvu ya kupambanua.

Suala La Sigara Ni La Kuzingatiwa

Suala la sigara na uvutaji wake ni la kuzinga­tiwa.

Ni kweli kuwa hatuwezi kuifananisha sigara na pombe au bangi, lakini hapana shaka kwamba mashirika ya kutengeneza sigara yanataka watu wazoee kuvuta sigara ili yapate faida na maslahi katika mauzo yao.

Katika nchi kadhaa zilizokuwa zikitawaliwa na Mwingereza, mkoloni alikuwa akimpa mtoto paketi moja ya sigara, kisha akimsimamisha na kumpiga picha ya haraka inayotoka Papohapo. Baadaye humpa mtoto huyo picha yake, paketi moja ya sigara na shilingi moja, na humwambia:

"Hii picha utaiweka kwenye albamu, paketi ya sigara utampa baba yako, na hiyo shilingi moja utanunua chochote unachopenda."

Kwa njia hii walikuwa wakiwazoesha wazazi kuvuta sigara, na kudhamini kwamba mtoto atakapokua naye atavuta sigara. Kwa sababu picha yake akiwa ameshika paketi ya sigara ita­mwathiri yenyewe na kuwa mvutaji.

Kwa hivyo, wanampata baba na mtoto.

Hivi ndivyo zilivyo zawadi za kikoloni, ni nzuri kwa nje tu, lakini kwa ndani ni udanga­nyifu mtupu.

Hapana budi tukumbuke kuwa wakoloni wa Kiingereza walikuwa wakiwalazimisha Wachina kulima bangi na kuitumia, na hata wakawaua maelfu yao waliopinga.

Ni marufuku katika Israel kulima bangi isipokuwa kwa wanaotaka kuingiza kimagendo katika ardhi za Kiarabu!

Kabla ya vita vya mwaka 1967 na 1973 kulikuwepo mpango wa magendo ya bangi kusafirisha kutoka Lebanon kupitia ardhi iliyokaliwa na Israel ambapo bangi ilikuwa ikifikishwa katika tambarare ya Baalbak kwenda katika mwambao wa Shaka, Betrun au Sidon, na huko ikipakiwa kwenye mashua kupelekwa katika Ras al-Dib, kusini mwa Akka. Huko magari ya Kiisraeli, aghlabu yao yakiwa na kijeshi, yali­kuwa yakingojea kuchukua mpaka kwenye bandari ya Elat au kwenye mapango ya jangwani. Kutoka huko ikasafirishwa kupitia kwenye vilima vya michanga hadi Sinai, na ngamia wakiwa ndio meli za jangwani husafirisha bangi katika Sinai. Kutoka Sinai inasafirishwa kwenda sehemu nyingine za Misri.

Basi baada ya hapo.......
Hayo huwa ndiyo sababu ya kuvuta bangi....
Na hayo ni matokeo yake....
Hivi sasa ulimwenguni kuna watu wapatao milioni mia nne wenye njaa ambao kuna hatari ya kufa wote katika miaka ijayo.
Na kuna watu wengine milioni mia nne wanaovuta bangi!

Kila mvuta bangi anavuta kila mwezi si chini ya bunda moja la bangi.

Ikiwa tutachukulia kila bunda moja la bangi gharama yake haipungui Pauni 22, hivyo, wavuta bangi wanatumia kiasi gani kwa mwezi?

Kwa ufupi, watakuwa wanatumia Pauni 8,800,000,000 kila mwezi ambayo ni sawa na Pauni 105,600,000,000 kwa mwaka - yaani zaidi ya bajeti za nchi zote za Kiarabu na Kiafrika!

Je, kiasi hiki hakiwezi kutumika kuwaokoa maskini kutokana na kifo katika kipindi cha miaka kumi?

Yapasa tuulizane: Kwa nini Mwenyezi Mungu ameharamisha pombe, bangi, heroini, kasumba na vileo vinginevyo?