read

Je, Mtume (s.a.w.) aliteuwa Mrithi?

“Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako, na ikiwa hutafanya hivyo, basi hukufikisha ujumbe wako ( kabisa); na Allah atakulinda na watu . Hakika Allah hawaongozi watu makafiri.”(Qr:5:67)
  
Mashia wanaamini kwamba tangazo lililotajwa na aya hiyo ya Qur’an hapo juu lilitimizwa na Mtume (s.a.w.) wakati alipomteua Imam ‘Ali bin Abi Talib (a.s.) kama mrithi wake katika siku ya Ghadir Khum.
 

Lakini je, neno Mawla lina maana ya Rafiki?

 
Ingawa idadi ya wanachuoni wa Ki-Sunni wazama zote na wa misimamo yote wamethibitisha tukio hili na maneno ya kihistoria ya Mtume (s.a.w.w) lakini wameona vigumu kulipatanisha na yaliyotokea haswa baada ya kifo cha Mtume (s.a.w). Ni nje ya upeo wa makala hii fupi kuyaelezea matukio haya kwa kinaganaga. Nukta muhimu ni kwamba wanachuoni wengi wa Ki-Sunni wanadai kwamba Mtume (s.a.w) alitaka tu kumtangaza ‘Ali (a.s) kwa Waislamu kama rafiki na msaidizi.
 
Kuna vipengele vingi kwenye tukio hili ambavyo huonyesha kwamba tukio hili lilikuwa na maana zaidi. Uteremshwaji wa aya mbali mbali za Qur’an, mkusanyiko mkubwa wa watu, hatua ya mwisho ya maisha ya Mtume (s.a.w), uthibitisho wa watu kwamba Mume s.a.w. alikuwa mbora na mkubwa katika mamlaka, na hatimaye hongera za Umar na halikadhalika mambo mengine mengi ambayo ni vigumu kueleza katika makala hii fupi nukta zote kwenye tukio hili kama moja ya utenzi wa mrithi uliofanywa na Mtume (s.a.w). Ni wazi kwamba neno ‘mawla’ lilitumika katika hali ya mamlaka kamili baada ya Mtume (s.a.w) bila kizuizi, pamoja na utawala wa kidunia.
 

Neno la Mwisho

 
Kama bado kumebakia shaka kuhusu umuhimu wa kihistoria wa maelezo haya na juhudi za baadhi ya watu ya kuyaandika, basi hili na liwe neno la mwisho:
 
Imam ‘Ali (a.s.) wakati wa kipindi chake cha Ukhalifa na miongo ya miaka baada ya tukio la Ghadir, alimuambia Anas bin Maliki Sahaba wa Mtume (s.a.w): “Kwa nini husimami na kuthibitisha kile ulichosikia kutoka kwa Mjumbe wa Allah (s.a.w) katika siku ya Ghadir?” Akajibu, “Ewe Amirul’Muminina! Nimekuwa mzee na sikumbuki.” Ambapo hapo Ali (a.s) alisema: “Allah akuweke alama ya baka jeupe ( la ukoma) lisilofichika kwa kilemba chako, kama kwa makusudi unaficha ukweli.” Na kabla Anas hajaamka kutoka sehemu yake aliyokaa, alipata baka kubwa jeupe katika uso wake.
 

Rejea

       Ibn Qutaybah al-Dinawar, Kitab al-Ma’rif, (Kairo 1353 A.H) uk. 251
       Ahmad bin Hanbal, al-Musnad, J. 1, uk, 119
       Abu Nu’aym al’Isfahani, Hilyat al-Awliya, (Beirut, 1988) J. 5. uk. 27
       Nur al-Din al-Halabi al-Shafii al-Sirah al-Halabiyya J. 3, uk. 336
       Al-Muttaqi al-Hindi, kaz al-Ummal,(Halab, 1969-84), J.13, uk.131
 
Kwa maelezo zaidi.
htt://al-islam.org/ghadir/
 
Translated by:
Dr M S Kanju
Al`Itrah Foundation
P O Box 1017
Dar es Salaam
Tanzania
Tel 255 22 2110640
Email alitrah@daiichicorp.com
Website www.alitrah.org