read

Raja'ah

Raja'ah: kwa Shi’a ina maana kwamba Mwenyezi Mungu atawarejesha katika siku za mwisho wa Dunia watu miongoni mwa wafu katika wale waliobobea katika imani na wale waliobobea katika ukafiri, Mwenyezi Mungu atalipiza kisasi hawa kwa wale.

Na itikadi hii sio muhimu sana katika madhehebu ya Shi’a na haina uzito kwa Shi’a ni kama vile imani juu ya Dajali na mambo mengine, amesema Kaashiful-Ghitrwaa.

Mmoja wa maulamaa wakubwa wa Kishi’a - kuamini raja'ah katika madhehebu la Shi’a sio lazima na wala kutoiamini kwake hakudhuru na wala Ushi’a haukuambatanishwa nayo kwa kuwepo au kutokuwepo kwake, nayo si kingine bali ni kama vile baadhi ya habari za ghaibu na matukio yajayo, masharti ya Qiyama mfano wa kushuka Isa kutoka mbinguni, kudhihiri Dajali, kutokea Sufiyani n.k. miongoni mwa mambo yaliyoenea kwa Waislamu nayo sio chochote katika Uislamu, kutoyaamini kwake sio kutoka katika Uislamu na wala kuyaamini kwake sio kuingia katika Uislamu, ndivyo ilivyo raja'ah."1

Na raja'ah ni mahala pa ikhitilafu baina ya maulamaa wa Kishi’a, kati yao wameithibitisha na kati yao kuna wanaoikanusha ...hakika raja'ah baadhi wameikuza na wakaihesabu kuwa ni katika misingi ya Ushi’a kwa uongo na uzushi.

Na raja'ah sio kwamba haiwezekani, baada ya kuwa ilishatokea katika kaumu zilizotangulia, katika Qur'an kuna sehemu nyingi kuhusu kurejea baadhi ya wafu katika uhai, mfano: "Uzair" ambaye Mwenyezi Mungu alimfisha miaka mia moja kisha akamfufua."2

Na wafuasi wa Musa waliotaka kumuona Mwenyezi Mungu, basi wakapatwa na mauti: Amesema Mwenyezi Mungu "Kisha tukawafufueni baada ya kufa kwenu huenda mtashukuru."3

Suyutwiy amesema kuhusu raja'ah lakini kwa maana inayotofautiana na waliyoisema Shi’a yeye amedai uwezekano wa kumuona Mtume (s.a.w.w) ukiwa macho, na ametunga kitabu juu ya hilo nacho ni "Imkaniyatu ru'uyatii Nabiyyi wal-malakati fiy yaqadhah (uwezekano wa kumuona Mtume na Malaika ukiwa macho). Na amedai kumuona kwake Mtume (s.a.w.w) zaidi ya mara Sabini akiwa macho.

Na amesema Aswabaan Ashaafiy kuhusu kurejea Mtume (s.a.w.w) baada ya kuzungumza juu ya njia za Isa kujua hukumu za Ki-Islamu baada ya kudhihiri kwake akasema: "Na kati ya njia hizo ni kwamba Isa atakaposhuka atakutana na Mtume (s.a.w.w) hivyo hakuna kizuizi cha kuchukua kutoka kwake anayoyahitaji kutoka kwake miongoni mwa hukumu za Kisheria."4
Amesema Dkt. Ali Abdul-wahlid Wafiy akitetea Shi’a: "Vyovyote iwavyo hakika kuitakidi kwa moja ya raja'ah mbili au zote mbili hakumtoi mwenye kuitakidi kwenye Uislamu."5

Baada ya safari hii fupi juu ya mawimbi ya kuvumbua zana iliyofichikana imetubainikia umuhimu wa madhehebu ya Ahlul-Bait (a.s) baina ya madhehebu zingine, umadhubuti wa misingi yake na ubora wa kujiunga nayo.

Pamoja na kwamba wapinzani wanaeneza uongo wa kuzua juu ya madhehebu ya Shi’a isipokuwa waadilifu katika maulamaa wa Ahlus-sunna wameandika wazi kuhusu kundi hili, baadhi yao wameyahesabu kuwa ni madhehbu ya tano na wakaifanya kuwa ni kioo cha mwisho cha Ki-Islamu kilicho safi na hizi ni baadhi ya kauli zao:

Imamul-Akbar Sheikhul - Azhari Mahmud Shaltut amesema: "Hakika madhehbu ya Ja'fariyah maarufu kama madhehebu ya Shi’atul-Imamiya; ni madhehebu yanayojuzu kufanya ibada ya Kisheria kwayo, kama madhehebu mengine ya Sunni."6

Sheikhul - Azhari Dkt. Muhammad Muhammad Al-Fahaam amesema: "Sheikh Shaltut mimi nilikuwa kati ya wanaovutiwa naye kwa tabia yake, elimu yake, upana wa fahamu yake na uwezo wake wa lugha ya Kiarabu, tafsiri ya Qur'an na kusomesha kwake Usulul-fiqihi, na ameshatoa fatwa juu ya hilo, yaani kujuzu kufanya ibada kwa mujibu wa madhehebu ya Shi’atul-Imamiyah - hapana shaka ametoa fatwa ambayo imejengeka juu ya msingi katika itikadi yangu. "7
Mwenyezi Mungu amrehemu Sheikh Shaltuti ambaye ametambua maana hii tukufu hivyo ukadumu katika fatwa yake ushujaa, kwa kujuzu kufanya amali kwa mujibu wa madhehbu ya Shi’a Imamiyah."8

Sheikh Muhammad al-Ghazaaliy amesema: Naitakidi kwamba fatwa ya Ustadh mkubwa Sheikh Mahmud Shaltut, imepiga hatua kubwa katika njia hii na mwanzo wa juhudi za mwenye ikhilasi miongoni mwa watu wenye mamlaka na wenye elimu wote, na ni ukanusho wa ambayo wanayatarajia makafiri wakimagharibi miongoni mwa chuki ambayo itauteketeza umma kabla ya kuungana na safu zake chini ya bendera moja ……fatwa hii kwa mtazamo wangu ni mwanzo wa njia na mwanzo wa vitendo.

Hakika Shi’a wanaamini ujumbe wa Muhammad na wanaona utukufu wa Ali upo katika kushikamana kwake na Sunna zake na wao ni kama Waislamu wengine.

Hawamuoni binadamu katika waliotangulia na katika wajao, mtukufu zaidi kuliko As-swadiqul-amini."9

Abdul-Rahmani Annajaar - mkurugenzi wa msikiti wa Cairo - amesema: "Fatwa ya Sheikh Shaltut tunatoa fatwa kwayo hivi sasa tunapoulizwa bila ya kujifunga na madhehbu manne, na Sheikh Shaltut ni Imam mujitahidi, rai yake inapatia ukweli halisi kwa nini tutosheke na fikra zetu na fatwa zetu juu ya madhehbu fulani tu, hali ya kuwa wote ni wenye kujitahidi."10

Dkt. Mustafa Raafiy amesema:
"Hayo madhehbu mawili (amekusudia Imamiyah na Zaidia) ya Ki-Islamu ambayo yanakutana pamoja na madhehbu ya Ahlus-sunna na inasihi kufanya ibada kulingana na hukumu zao; na sioni ambayo yanazuia kuitakidi madhehebu ya Ja’fariyah sambamba na madhehebu manne."11

Hasan al-Banaa amesema:
Tambueni kwamba Sunni na Shi’a ni Waislamu; linawakusanya neno la "Laa Ilaaha Illa-llaahu wa Anna Muhammadan Rasulu llaahi" na huu ni msingi wa itikadi, na Sunni na Shi’a hapo wako sawa na hapo ndipo wanapokutanika, ama tofauti baina yao ni katika mambo ambayo kuna uwezekano wa kukurubiana baina yao.12

Ustadh Ahmad Beka Al-Masriy, Ustadh Shaltuti na Abu Zahra, amesema, "Shi’atul-imamiyah ni waislamu, wanamwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Qur'ani na yote ambayo alikuja nayo Muhammad (s.a.w.w), na katika Shi’a Imamiyah, zamani na hivi sasa kuna mafaqihi wakubwa sana na maulamaa katika kila fani na wao wanafikra za kina, wapana wa maarifa na utunzi wao unahesabiwa kwa mamia ya maelfu na nimeshasoma mwingi miongoni mwao."13

Sheikhul-Azhar Sayid Muhammad Twantawiy amesema: "Hakika waislamu Sunni na Shi’a wanamuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kwamba tofauti za maoni hazipunguzi daraja ya imani za watu."14

Ustadh Mahamud As-Sartwawiy - mkuu wa kitivo cha sheria katika Chuo kikuu cha Jordan na mmoja kati ya watoa fatwa wakuu anasema:

"Hakika mimi nasema ambayo wanayasema: Shi’a Imamiyah ni ndugu zetu katika dini, wanao kwetu haki ya udugu na tunao kwao mfano wa waliyonayo kwetu, yanayopatikana baina yetu na wao miongoni mwa tofauti za maoni hakika ni katika matawi."15

Ustadh Abdul-Fataha AbdulMaqsd anasema:
"Hakika katika itikadi yangu ni kwamba Shi’a wao ni picha ya uislamu sahihi na ni kioo safi na anayetaka kutazama Uislam ni juu yake atazame kupitia itikadi ya Shi’a na kupitia katika vitendo vyao, na historia ni shahidi bora juu ya ambayo wanayafanya Shi’a miongoni mwa huduma kubwa katika uwanja wa kutetea itikadi ya Ki-Islamu.
Na hakika maulamaa wa Kishi’a watukufu ndio ambao wameshika nafasi kubwa ambayo hajaishika yeyote asiyekuwa wao katika nyanja mbali mbali, wamepigana, wamepambana na wamejitoa muhanga kwa ajili ya kuunyanyua Uislamu na kueneza mafunzo yake matukufu, kuwaelimisha watu na kuwaelekeza kwenye Qur'an."16

 • 1. AswiluShiatu wa usuluha uk. 68
 • 2. Suratul- Baqarah: 259
 • 3. Suratul- Baqarah: 56
 • 4. Is'afu-raghibiyna bihaamishi nurul-abswar 161
 • 5. Baina Shiati wa Ahlus-sunnah uk. 57
 • 6. Islamunaa cha Raafiy uk. 59 na ilitangazwa katika jarida la Risaatul-islamu linalochapishwa Misri
 • 7. Fiy sabil-wahdatil - islaamiyah cha Ridhawiy uk
 • 8. Islamuna:59
 • 9. Difaain anil aqiida Uk. 257
 • 10. Fiy sabil wahdahti Islaamiyati cha Murtadha Ridhwi uk:
 • 11. Islaamuna a uk:32 59
 • 12. Dhikriyaatu laa mudhakaraatu cha omar Tilmisaaniy uk: 249, jarida la Al- alam toleo NO: 519 uk : 40
 • 13. Tarekh tashiriul Islam
 • 14. Majalatu thaqalain toleo la pili mwaka wa kwanza - 1413H uk: 252 na 253.
 • 15. Majalatu thaqalain toleo la pili mwaka wa kwanza - 1413H uk: 90
 • 16. Fiy sabilil-wahdatil - islaamyat